Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 3:4-18 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 3:4-18 in Biblia Takatifu

4 Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni mapito yake.
5 Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyooshwa, njia mbaya zitatengenezwa.
6 Na, watu wote watauona wokovu utokao kwa Mungu.”
7 Basi, Yohane akawa anawaambia watu wengi waliofika ili awabatize: “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mngeweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
8 Basi, onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kusema: Sisi ni watoto wa Abrahamu. Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyageuza mawe haya yawe watoto wa Abrahamu!
9 Lakini, sasa hivi shoka limewekwa tayari kukata mizizi ya miti. Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni.”
10 Umati wa watu ukamwuliza, “Tufanye nini basi?”
11 Akawajibu, “Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo.”
12 Nao watoza ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza, “Mwalimu, tufanye nini?”
13 Naye akawaambia, “Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa.”
14 Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanye nini?” Naye akawajibu, “Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu.”
15 Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusu Yohane: kuwa labda yeye ndiye Kristo.
16 Hapo Yohane akawaambia wote, “Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia kamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17 Yeye ni kama mtu anayeshika mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka, aipure nafaka yake, akusanye ngano ghalani mwake, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
18 Hivyo, pamoja na mawaidha mengine mengi, Yohane aliwahimiza watu akiwahubiria Habari Njema.
Luka 3 in Biblia Takatifu

Luka 3:4-18 in Biblia ya Kiswahili

4 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya Isaya nabii, “sauti ya mtu aliaye nyikani, “Itengenezeni tayari njia ya Bwana, yatengenezeni mapito yake yaliyoonyoka.
5 Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa, barabara zilizopinda zitanyoshwa, na njia zilizoparaza zitalainishwa.
6 Watu wote watauona wokovu wa Mungu.”
7 Hivyo, Yohana akawaambia makutano makubwa ya watu waliomjia wapate kubatizwa na yeye, “Ninyi uzao wa nyoka wenye sumu, nani aliwaonya kuikimbia gadhabu inayokuja?
8 Zaeni matunda yanayoedana na toba, na msianze kusema ndani yenu, “Tunaye Ibarahimu ambaye ni baba yetu; kwa sababu nawaambia ya kwamba, Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutokana na mawe haya.
9 Tayari shoka limeshawekwa kwenye mzizi wa miti. Hivyo, kila mti usiozaa matunda mema, hukatwa na kutupwa motoni.
10 Kisha watu katika makutano walimuuliza wakisema, “Sasa tunatakiwa tufanyeje?”
11 Alijibu na kuwaambia, “kama mtu ana kanzu mbili anatakiwa atoe kanzu moja kwa mwingine ambaye hana kabisa, na ambaye ana chakula na afanye vivyo hivyo.”
12 Kisha baadhi ya watoza ushuru walikuja pia kubatizwa, na wakamwambia, “Mwalimu, tunatakiwa kufanya nini?
13 Akawaambia, “Msikusanye fedha zaidi kuliko mnachotakiwa kukusanya.”
14 Baadhi ya maaskari pia wakamuuliza wakisema, “Na sisi je? Tunatakiwa tufanye nini?” Akawambia, “Msichukue fedha kwa mtu yeyote kwa nguvu, na msimtuhumu mtu yeyote kwa uongo. Ridhikeni na mishahara yenu.”
15 Sasa, kwa kuwa watu walikuwa na shauku ya kumngojea Kristo atakaye kuja, kila mmoja alikuwa anawaza moyoni mwake kuhusu Yohana kama yeye ndiye Kristo.
16 Yohana akajibu kwa kuwaambia wote, “Mimi nawabatiza ninyi kwa maji, lakini kuna mmoja ajaye ambaye ana nguvu kuliko mimi, na sisitahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17 Pepeto lake liko mkononi mwake ili kusafisha vizuri uwanda wake wa kupepetea ngano na kuikusanya ngano ghalani mwake. Lakini, atayateketeza makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.
18 Kwa maonyo mengine mengi pia, alihubiri habari njema kwa watu.
Luka 3 in Biblia ya Kiswahili