3 Alisafiri katika mkoa wote kuzunguka Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi
4 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya Isaya nabii, “sauti ya mtu aliaye nyikani, “Itengenezeni tayari njia ya Bwana, yatengenezeni mapito yake yaliyoonyoka.
5 Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa, barabara zilizopinda zitanyoshwa, na njia zilizoparaza zitalainishwa.
6 Watu wote watauona wokovu wa Mungu.”
7 Hivyo, Yohana akawaambia makutano makubwa ya watu waliomjia wapate kubatizwa na yeye, “Ninyi uzao wa nyoka wenye sumu, nani aliwaonya kuikimbia gadhabu inayokuja?
8 Zaeni matunda yanayoedana na toba, na msianze kusema ndani yenu, “Tunaye Ibarahimu ambaye ni baba yetu; kwa sababu nawaambia ya kwamba, Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutokana na mawe haya.
9 Tayari shoka limeshawekwa kwenye mzizi wa miti. Hivyo, kila mti usiozaa matunda mema, hukatwa na kutupwa motoni.
10 Kisha watu katika makutano walimuuliza wakisema, “Sasa tunatakiwa tufanyeje?”