Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 1:3-11 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 1:3-11 in Biblia Takatifu

3 Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango,
4 ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa.
5 Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni.
6 Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.
7 Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana.
8 Siku moja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu,
9 Zakariya alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani.
10 Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani.
11 Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani.
Luka 1 in Biblia Takatifu

Luka 1:3-11 in Biblia ya Kiswahili

3 Hivyo nami pia, baada ya kuchuguza kwa uangalifu chanzo cha mambo haya yote tokea mwanzo - nimeona ni vema kwangu pia kukuandikia katika mpangilio wake - mheshimiwa sana Theofilo.
4 Ili kwamba uweze kujua ukweli wa mambo uliyofundishwa.
5 Katika siku za Herode, mfalme wa Yudea, palikuwa na kuhani fulani aliyeitwa Zekaria, wa ukoo wa Abiya. Mke wake alitoka kwa binti za Haruni, na jina lake aliitwa Elizabeti.
6 Wote walikuwa wenye haki mbele za Mungu; walitembea bila lawama katika amri zote na maagizo ya Bwana.
7 Lakini hawakuwa na mtoto, kwasababu Elizabethi alikuwa tasa, na kwa wakati huu wote wawili walikuwa wazee sana.
8 Sasa ilitokea kwamba Zakaria alikuwa katika uwepo wa Mungu, akiendelea na wajibu wa kikuhani katika utaratibu wa zamu yake.
9 Kulingana na desturi ya kuchagua ni kuhani yupi atakayehudumu, alikuwa amechaguliwa kwa kura kuingia katika hekalu la Bwana na hivyo angefukiza uvumba.
10 Kundi lote la watu lilikuwa likiomba nje wakati wa kufukizwa kwa ufumba.
11 Sasa malaika wa Bwana alimtokea na kasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia.
Luka 1 in Biblia ya Kiswahili