Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 1:18-30 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 1:18-30 in Biblia Takatifu

18 Zakariya akamwambia huyo malaika, “Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu.”
19 Malaika akamjibu, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu, na nimetumwa niseme nawe, nikuletee hii habari njema.
20 Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia.”
21 Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakariya huku wakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni.
22 Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono Hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu.
23 Zamu yake ya kuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani.
24 Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba. Akajificha nyumbani kwa muda wa miezi mitano, akisema:
25 “Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana; ameniangalia na kuniondolea aibu niliyokuwa nayo mbele ya watu.”
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya,
27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi.
28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.”
29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini?
30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema.
Luka 1 in Biblia Takatifu

Luka 1:18-30 in Biblia ya Kiswahili

18 Zakaria akamwambia malaika, “Nitawezaje kujua hili? Kwasababu mimi ni mzee na mke wangu miaka yake imekuwa mingi sana.”
19 Malaika akajibu na kumwambia, “Mimi ni Gabrieli, ambaye husimama mbele za Mungu. Nilitumwa kukwambia, kukuletea habari hii njema.
20 Na tazama, hutaongea, utakuwa kimya, hutaweza kuongea mpaka siku ile mambo haya yatakapotokea. Hii ni kwasababu ulishindwa kuamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati mwafaka.”
21 Sasa watu walikuwa wakimsubiri Zakaria. Walishangazwa kwamba alikuwa anatumia muda mwingi hekaluni.
22 Lakini alipotoka nje, hakuweza kuongea nao. Wakatambua kwamba alikuwa amepata maono alipokuwa hekaluni. Aliendelea kuonesha ishara na alibaki kimya.
23 Ikatokea kwamba siku za huduma yake zilipokwisha aliondoka kurudi nyumbani kwake.
24 Baada ya Zakaria kurudi nyumbani kutoka kwenye huduma yake hekaluni, mke wake akawa mjamzito. Naye hakutoka nyumbani mwake kwa muda wa miezi mitano. Akasema,
25 “Hili ndilo amabalo Bwana amefanya kwangu aliponitazama kwa upendeleo ili kuiondoa aibu yangu mbele za watu.”
26 Sasa, katika mwezi wa sita wa mimba ya Elizabeti, Mungu alimwambia malaika Gabrieli kwenda kwenye mji wa Galilaya uitwao Nazareti,
27 kwa bikra aliyekuwa ameposwa na mwanaume ambaye jina lake lilikuwa Yusufu. Yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi, na jina la bikra huyo lilikuwa Mariamu.
28 Akaja kwake na akasema, “Salaam, wewe uliyepokea neema kuu! Bwana amependezwa nawe.”
29 Lakini maneno ya malaika yalimchanganya na hakuelewa kwa nini malaika alisema salaam hii ya ajabu kwake.
30 Malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu, maana umepata neema kutoka kwa Mungu.
Luka 1 in Biblia ya Kiswahili