Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 18:25-35 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 18:25-35 in Biblia Takatifu

25 Naam, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”
26 Wale watu waliposikia hayo, wakasema, “Nani basi, atakayeokolewa?”
27 Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa binadamu, yanawezekana kwa Mungu.”
28 Naye Petro akamwuliza, “Na sisi je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!”
29 Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, mtu yeyote aliyeacha nyumba au mke au kaka au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,
30 atapokea mengi zaidi wakati huu wa sasa, na kupokea uzima wa milele wakati ujao.”
31 Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa.
32 Kwa maana atakabidhiwa kwa watu wa mataifa nao watamtendea vibaya na kumtemea mate.
33 Watampiga mijeledi, watamuua; lakini siku ya tatu atafufuka.”
34 Lakini wao hawakuelewa hata kidogo jambo hilo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.
35 Wakati Yesu alipokaribia Yeriko, kulikuwa na mtu mmoja kipofu ameketi njiani akiomba.
Luka 18 in Biblia Takatifu

Luka 18:25-35 in Biblia ya Kiswahili

25 Maana ni rahisi sana kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.'
26 Wale waliosikia hayo, wakasema, 'Nani basi, atakayeweza kuokolewa?'
27 Yesu akajibu, 'Mambo yasiyowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yanawezekana.”
28 Petro akasema, 'Naam, sisi tumeacha kila kitu na tumekufuata wewe.'
29 Kisha Yesu akawaambia, Amin, nawaambia kwamba hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto, kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,
30 ambaye hatapokea mengi zaidi katika ulimwengu huu, na katika ulimwengu ujao, uzima wa milele.'
31 Baada ya kuwakusanya wale kumi na wawibili, akawaambia, 'Tazama, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote ambayo yameandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Adamu yatakamilishwa.
32 Kwa maana atatiwa mikononi mwa watu wa Mataifa na atatendewa dhihaka na jeuri, na kutemewa mate.
33 Baada ya kumchapa viboko watamwua na siku ya tatu atafufuka.'
34 Hawakuelewa mambo haya, na neno hili lilikuwa limefichwa kwao, na hawakuelewa mambo yaliyosemwa.
35 Ikawa Yesu ulipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya barabara akiomba msaada,
Luka 18 in Biblia ya Kiswahili