Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 14:3-32 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 14:3-32 in Biblia Takatifu

3 Yesu akawauliza walimu wa Sheria na Mafarisayo, “Je, ni halali au la kumponya mtu siku ya sabato?”
4 Lakini wao wakakaa kimya. Yesu akamshika huyo mgonjwa, akamponya, akamwacha aende zake.
5 Halafu akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye mtoto wake au ng'ombe wake akitumbukia shimoni, hangemtoa hata kama ni siku ya Sabato?”
6 Nao hawakuweza kumjibu swali hilo.
7 Yesu aliona jinsi wale walioalikwa walivyokuwa wanajichagulia nafasi za heshima, akawaambia mfano:
8 “Kama mtu akikualika arusini, usiketi mahali pa heshima isije ikawa amealikwa mwingine mheshimiwa kuliko wewe;
9 na mwenyeji wenu ninyi wawili atakuja na kukwambia: Mwachie huyu nafasi. Hapo utaaibika mbele ya wote na kulazimika kwenda kuchukua nafasi ya mwisho.
10 Bali ukialikwa kwenye karamu, keti mahali pa mwisho, ili mwenyeji wako atakapokuja akwambie: Rafiki, njoo hapa mbele, mahali pazuri zaidi. Hapo utakuwa umeheshimika mbele ya wote wanaoketi pamoja nawe.
11 Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa, na anayejishusha, atakwezwa.”
12 Halafu akamwambia na yule aliyemwalika, “Kama ukiwaandalia watu karamu mchana au jioni, usiwaalike rafiki zako au jamaa zako au jirani zako walio matajiri, wasije nao wakakualika nawe ukawa umelipwa kile ulichowatendea.
13 Badala yake, unapofanya karamu, waalike maskini, vilema viwete na vipofu,
14 nawe utakuwa umepata baraka, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa. Maana Mungu atakupa tuzo lako wakati watu wema watakapofufuka.”
15 Mmoja wa wale waliokuwa wameketi pamoja na Yesu akasema, “Ana heri mtu yule atakayekula chakula katika Ufalme wa Mungu.”
16 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu wengi.
17 Wakati wa karamu ulipofika alimtuma mtumishi wake awaambie walioalikwa, Njoni, kila kitu ni tayari.
18 Lakini wote, kwa namna moja, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi: Nimenunua shamba, kwa hiyo sina budi kwenda kuliangalia; nakuomba uniwie radhi.
19 Mwingine akasema: Nimenunua ng'ombe jozi tano wa kulima; sasa nimo njiani kwenda kuwajaribu; nakuomba uniwie radhi.
20 Na mwingine akasema: Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.
21 Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule mwenye nyumba alikasirika, akamwambia mtumishi wake: Nenda upesi kwenye barabara na vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete, vipofu na waliolemaa.
22 Baadaye, mtumishi huyo akasema: Bwana mambo yamefanyika kama ulivyoamuru, lakini bado iko nafasi.
23 Yule bwana akamwambia mtumishi: Nenda katika barabara na vichochoro vya mji uwashurutishe watu kuingia ili nyumba yangu ijae.
24 Kwa maana, nawaambieni, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa atakayeonja karamu yangu.”
25 Hapo, makundi mengi yakawa yanaandamana pamoja na Yesu. Basi, akawageukia akawaambia,
26 “Mtu yeyote akija kwangu, asipowachukia baba na mama yake, mke wake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 Mtu asipochukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28 Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia?
29 La sivyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, watu watamcheka
30 wakisema: Mtu huyu alianza kujenga, lakini hakumalizia.
31 “Au, ni mfalme gani ambaye, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza chini na kufikiri kama ataweza, kwa askari wake elfu ishirini?
32 Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
Luka 14 in Biblia Takatifu

Luka 14:3-32 in Biblia ya Kiswahili

3 Yesu aliuliza wataalam katika sheria ya Wayahudi na Mafarisayo, “Je, ni halali kumponya siku ya Sabato, au sivyo?”
4 Lakini wao walikuwa kimya, kwahiyo Yesu akamshika, akamponya na kumruhusu aende zake.
5 Naye akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye ana mtoto au ng'ombe anatumbukia kisimani siku ya Sabato hata mvuta nje mara moja?”
6 Wao hawakuwa na uwezo wa kutoa jibu kwa mambo haya.
7 Wakati Yesu alipogundua jinsi wale walioalikwa kwamba wamechagua viti vya heshima, akawaambia mfano, akiwaambia,
8 “Wakati mnapoalikwa na mtu harusini, usiketi katika nafasi za heshima, kwa sababu inawezekana amealikwa mtu ambaye ni wakuheshimiwa zaidi kuliko wewe.
9 Wakati mtu aliyewaalika ninyi wawili akifika, atakuambia wewe, “mpishe mtu huyu nafasi yako,” na kisha kwa aibu utaanza kuchukua nafasi ya mwisho.
10 Lakini wewe ukialikwa, nenda ukakae mahali pa mwisho, ili wakati yule aliyekualika akija, aweze kukuambia wewe, `Rafiki, nenda mbele zaidi.” ndipo utakuwa umeheshimika mbele ya wote walioketi pamoja nawe mezani.
11 Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa, na yeye ajishushae atakwezwa.'
12 Yesu pia alimwambia mtu aliyemwalika, 'Unapotoa chakula cha mchana au cha jioni, usiwaalike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako matajiri, ili kwamba wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.
13 Badala yake, unapofanya sherehe, waalike maskini, vilema, viwete na vipofu,
14 na wewe utabarikiwa, kwa sababu hawawezi kukulipa. Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.”
15 Wakati mmoja wa wale walioketi mezani pamoja na Yesu aliposikia hayo, naye akamwambia, “Amebarikiwe yule atakayekula mkate katika Ufalme wa Mungu!”
16 Lakini Yesu akamwambia, “Mtu mmoja aliandaa sherehe kubwa, akaalika watu wengi.
17 Wakati sherehe ilipokuwa tayari, alimtuma mtumishi wake kuwaambia wale walioalikwa, `'Njooni, kwa sababu vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.'
18 Wote, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi, 'Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali unisamehe.'
19 Na mwingine akasema, `'Nimenunua jozi tano za ng'ombe, na mimi naenda kuwajaribu. Tafadhali uniwie radhi.'
20 Na mtu mwingine akasema, 'Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.'
21 Mtumishi akarudi na kumwambia bwana wake mambo hayo. Yule mwenye nyumba alikasirika akamwambia mtumishi wake, `'Nenda upesi mitaani na katika vichochoro vya mji ukawalete hapa maskini, vilema, vipofu na walemavu.”
22 Mtumimishi akasema, `Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa bado kuna nafasi.'
23 Bwana akamwambia mtumishi, 'Nenda katika njia kuu na vichochoro na uwashurutishe watu waingie, ili nyumba yangu ijae.
24 Kwamaana nawaambia, katika wale walioalikwa wa kwanza hapana atakayeonja sherehe yangu.'
25 Sasa umati mkubwa walikuwa wanakwenda pamoja naye, naye akageuka na akawaambia,
26 'Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, mama yake, mke wake, watoto wake, ndugu zake waume na wanawake- ndio, na hata maisha yake pia -hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 Mtu asipochukua msalaba wake na kuja nyuma yangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28 Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo?
29 Vinginevyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, wote walioona wataanza kumdhihaki,
30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.'
31 Au mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine katika vita, ambae hatakaa chini kwanza na kuchukua ushauri kuhusu kama ataweza, pamoja na watu elfu kumi kupigana na mfalme mwingine anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
32 Na kama sivyo, wakati jeshi la wengine bado liko mbali, hutuma balozi kutaka masharti ya amani.
Luka 14 in Biblia ya Kiswahili