8 Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
9 Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu.
10 Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa.
11 Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wanye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema,
12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo.”
13 Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu.”
14 Yesu akamjibu, ni nani aliye niweka kuwa mwamuzi na mpatanishi kati yenu.?
15 Ndipo akawaambia, Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.”
16 Yesu akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana,
17 na akajiuliza ndani yake, akisema, nitafanyaje kwani sina mahali pa kuhifadhi mazao yangu?
18 Akasema, nitafanya hivi. Nitavunja ghala zangu ndogo na kujenga iliyo kubwa, na kuyahifadhi mazao yangu yote na vitu vingine.
19 Nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, umejiwekea akiba ya vitu vingi kwa miaka mingi. Pumzika, ule, unywe na kustarehe.”
20 Lakini Mungu akamwambia, ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho kutoka kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini?
21 Ndivyo itakavyokuwa kwa kila mtu anayejiwekea mali na si kujitajirisha kwa ajili ya Bwana.
22 Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kwa hiyo nawaambia msihofu juu ya maisha yenu__ya kuwa mtakula nini au juu ya miili yenu __ya kuwa mtavaa nini
23 Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
24 Angalieni ndege wa angani, hawalimi wala hawavuni. Hawana chumba wala ghala ya kuhifadhia, lakini Baba yenu huwalisha. Ninyi si bora zaidi kuliko ndege!
25 Ni yupi kati yenu ambaye akijisumbua ataweza kuongeza dhiraa moja katika maisha yake?
26 Ikiwa basi hamuwezi kufanya hicho kitu kidogo kilicho rahisi kwa nini basi kusumbukia hayo mengine?.