Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 12:31-57 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 12:31-57 in Biblia Takatifu

31 Shughulikieni kwanza Ufalme wa Mungu, na hayo yote mtapewa kwa ziada.
32 “Msiogope, enyi kundi dogo! Maana Baba yenu amependa kuwapeni Ufalme.
33 Uzeni mali yenu mkawape maskini misaada. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, na jiwekeeni hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii, wala nondo hawaharibu.
34 Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.
35 “Muwe tayari! Jifungeni mkanda kiunoni, na taa zenu ziwe zinawaka;
36 muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka arusini, ili wamfungulie mara atakapobisha hodi.
37 Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni, atawaketisha mezani na kuwahudumia.
38 Heri yao watumishi hao ikiwa bwana wao atawakuta wanakesha hata ikiwa atarudi usiku wa manane au alfajiri.
39 Jueni kwamba, kama mwenye nyumba angejua saa ambayo mwizi atakuja, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
40 Nanyi, kadhalika muwe tayari, maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.”
41 Petro akamwambia, “Bwana, mfano huo ni kwa ajili yetu tu, au ni kwa ajili ya watu wote?”
42 Bwana akajibu, “Ni nani basi, mtumishi aliye mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wake ili awape chakula wakati ufaao?
43 Heri yake mtumishi huyo ikiwa bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo.
44 Hakika atampa madaraka juu ya mali yake yote.
45 Lakini, kama mtumishi huyo atafikiri moyoni mwake: na kusema: Bwana wangu amekawia sana kurudi halafu aanze kuwapiga watumishi wenzake, wa kiume au wa kike, na kula, kunywa na kulewa,
46 bwana wake atarudi siku asiyoitazamia na saa asiyoijua; atamkatilia mbali na kumweka fungu moja na wasioamini.
47 Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana.
48 Lakini yule afanyaye yanayostahili adhabu bila kujua, atapigwa kidogo. Aliyepewa vingi atatakiwa vingi; aliyekabidhiwa vingi zaidi atatakiwa kutoa vingi zaidi.
49 “Nimekuja kuwasha moto duniani, laiti ungekuwa umewaka tayari!
50 Ninao ubatizo ambao inanipasa niupokee; jinsi gani ninavyohangaika mpaka ukamilike!
51 Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? Hata kidogo; si amani bali utengano.
52 Na tangu sasa, jamaa ya watu watano itagawanyika; watatu dhidi ya wawili, na wawili dhidi ya watatu.
53 Baba atakuwa dhidi ya mwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mama dhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake; mama mkwe dhidi ya mke wa mwanawe na huyo dhidi ya mama mkwe wake.”
54 Yesu akayaambia tena makundi ya watu, “Mnapoona mawingu yakitokea upande wa magharibi, mara mwasema: Mvua itanyesha, na kweli hunyesha.
55 Mnapoona upepo wa kusi unavuma, mwasema Kutakuwa na hali ya joto na ndivyo inavyokuwa.
56 Enyi wanafiki! Mnajua kutabiri hali ya hewa kwa kuangalia dunia na anga; kwa nini basi, hamwezi kujua maana ya nyakati hizi?
57 “Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya?
Luka 12 in Biblia Takatifu

Luka 12:31-57 in Biblia ya Kiswahili

31 Lakini tafuteni ufalme wake kwanza, na hayo mengine mtazidishiwa,
32 msiogope, enyi kundi dogo, kwa sababu Baba yenu anafurahia kuwapa ninyi huo ufalme.
33 Uzeni mali zenu na mkawape maskini, mjifanyie mifuko isiyoishiwa__hazina ya mbinguni isiyokoma, sehemu ambapo wezi hawatakaribia wala nondo haitaweza kuharibu.
34 Kwa kuwa palipo na hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwepo.
35 Nguo zenu ndefu ziwe zimefungwa kwa mkanda, na taa zenu zihakikishwe kuwa zinaendelee kuwaka,
36 na muwe kama watu wanaomtazamia Bwana wao kutoka kwenye sherehe ya harusi, ili kwamba akija na kupiga hodi, wataweze kumfungulia mlango kwa haraka.
37 Wamebarikiwa wale watumishi, ambao Bwana atawakuta wako macho. Hakika atafunga nguo yake ndefu kwa mkanda, kisha atawaketisha chini kwa chakula, na kisha kuwahudumia.
38 Kama Bwana atakuja kwa zamu ya pili ya ulinzi ya usiku, au hata zamu ya tatu ya ulinzi, na kuwakuta wakiwa tayari, itakuwa ni heri kwa hao watumishi.
39 Zaidi ya hayo, mjue hili, kama bwana mwenye nyumba angelijua saa ambayo mwivi anakuja, asingeliruhusu nyumba yake ifunjwe.
40 Iweni tayari pia kwani hamjui ni wakati gani mwana wa Adamu atarudi.
41 Petro akasema, “Bwana, watuambia sisi wenyewe hii mifano, au unamwambia kila mtu.?
42 Bwana akawaambia, “Ni nani mtumwa mwaminifu au mwenye hekima ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wengine, ili awagawie chakula chao kwa wakati mwafaka?
43 Amebarikiwa mtumishi yule, ambaye bwana wake akija atamkuta akifanya yale aliyoagizwa.
44 Hakika nawaambia ninyi ya kuwa atamweka juu ya mali yake yote.
45 Lakini Mtumishi yule akisema moyoni mwake, “bwana wangu anachelewa kurudi; hivyo akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, kisha akaanza kula, kunywa na kulewa,
46 bwana wake yule mtumwa atakuja katika siku asiyotegemea na saa asiyoijua, naye atamkata vipande vipande na kumuweka katika sehemu pamoja na wasiokuwawaaminifu'
47 Mtumishi, anayejua mapenzi ya bwana wake, naye hakujiandaaa wala hakufanya sawa sawa na mapenzi yake, atapigwa viboko vingi.
48 Lakini mtumishi asiyejua mapenzi ya bwana wake, lakini akafanya yanayostahili adhabu, atapigwa viboko vichache. Kwa kuwa yeye aliyepewa vingi, vingi hudaiwa kutoka kwake, na yeye aliyeaminiwa kwa vingi, kwake vitadaiwa vingi zaidi.
49 Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka,
50 Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utkapokamilika!
51 Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, Nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko.
52 Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu.
53 Watagawanyika, baba atakuwa kinyume na mwanae, na mwanae atakuwa kinyume na babaye, mama atakuwa kinyume na binti yake, na binti atakuwa kinyume na mama yake, Mama mkwe atakuwa kinyume na mkwe wake naye mkwe atakuwa kinyume na mama mkwe wake.
54 Yesu akawa anawaambia makutano pia, “Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema nyakati za mvua zimewadia; na ndivyo inavyo kuwa,
55 Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, Patakuwepo na joto kali, na ndivyo inavyokuwa.
56 Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo?
57 Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo?
Luka 12 in Biblia ya Kiswahili