Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 12:25-42 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 12:25-42 in Biblia Takatifu

25 Ni nani kati yenu kwa kuwa na wasiwasi anaweza kuongeza urefu wa maisha yake?
26 Basi, kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini kuwa na wasiwasi juu ya yale mengine?
27 Angalieni maua jinsi yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayafumi. Hata hivyo, nawahakikishieni kwamba hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.
28 Lakini, kama Mungu hulivika vizuri jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, je, hatawafanyia ninyi zaidi? Enyi watu wenye imani haba!
29 “Basi, msivurugike akili, mkihangaika daima juu ya mtakachokula au mtakachokunywa.
30 Kwa maana hayo yote ndiyo yanayohangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo.
31 Shughulikieni kwanza Ufalme wa Mungu, na hayo yote mtapewa kwa ziada.
32 “Msiogope, enyi kundi dogo! Maana Baba yenu amependa kuwapeni Ufalme.
33 Uzeni mali yenu mkawape maskini misaada. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, na jiwekeeni hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii, wala nondo hawaharibu.
34 Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.
35 “Muwe tayari! Jifungeni mkanda kiunoni, na taa zenu ziwe zinawaka;
36 muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka arusini, ili wamfungulie mara atakapobisha hodi.
37 Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni, atawaketisha mezani na kuwahudumia.
38 Heri yao watumishi hao ikiwa bwana wao atawakuta wanakesha hata ikiwa atarudi usiku wa manane au alfajiri.
39 Jueni kwamba, kama mwenye nyumba angejua saa ambayo mwizi atakuja, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
40 Nanyi, kadhalika muwe tayari, maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.”
41 Petro akamwambia, “Bwana, mfano huo ni kwa ajili yetu tu, au ni kwa ajili ya watu wote?”
42 Bwana akajibu, “Ni nani basi, mtumishi aliye mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wake ili awape chakula wakati ufaao?
Luka 12 in Biblia Takatifu

Luka 12:25-42 in Biblia ya Kiswahili

25 Ni yupi kati yenu ambaye akijisumbua ataweza kuongeza dhiraa moja katika maisha yake?
26 Ikiwa basi hamuwezi kufanya hicho kitu kidogo kilicho rahisi kwa nini basi kusumbukia hayo mengine?.
27 Angalieni maua -yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya,
28 Kama Mungu huyavika vizuri majani ya kondeni, ambayo leo yapo, na kesho hutupwa kwenye moto. Je si zaidi atawavika ninyi? enyi wa imani haba!
29 Msisumbukie juu ya kuwa mtakula nini au mtakunywa nini, wala msiwe na hofu.
30 Kwa kuwa Mataifa yote ya dunia husumbukia mambao yao. Na Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo.
31 Lakini tafuteni ufalme wake kwanza, na hayo mengine mtazidishiwa,
32 msiogope, enyi kundi dogo, kwa sababu Baba yenu anafurahia kuwapa ninyi huo ufalme.
33 Uzeni mali zenu na mkawape maskini, mjifanyie mifuko isiyoishiwa__hazina ya mbinguni isiyokoma, sehemu ambapo wezi hawatakaribia wala nondo haitaweza kuharibu.
34 Kwa kuwa palipo na hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwepo.
35 Nguo zenu ndefu ziwe zimefungwa kwa mkanda, na taa zenu zihakikishwe kuwa zinaendelee kuwaka,
36 na muwe kama watu wanaomtazamia Bwana wao kutoka kwenye sherehe ya harusi, ili kwamba akija na kupiga hodi, wataweze kumfungulia mlango kwa haraka.
37 Wamebarikiwa wale watumishi, ambao Bwana atawakuta wako macho. Hakika atafunga nguo yake ndefu kwa mkanda, kisha atawaketisha chini kwa chakula, na kisha kuwahudumia.
38 Kama Bwana atakuja kwa zamu ya pili ya ulinzi ya usiku, au hata zamu ya tatu ya ulinzi, na kuwakuta wakiwa tayari, itakuwa ni heri kwa hao watumishi.
39 Zaidi ya hayo, mjue hili, kama bwana mwenye nyumba angelijua saa ambayo mwivi anakuja, asingeliruhusu nyumba yake ifunjwe.
40 Iweni tayari pia kwani hamjui ni wakati gani mwana wa Adamu atarudi.
41 Petro akasema, “Bwana, watuambia sisi wenyewe hii mifano, au unamwambia kila mtu.?
42 Bwana akawaambia, “Ni nani mtumwa mwaminifu au mwenye hekima ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wengine, ili awagawie chakula chao kwa wakati mwafaka?
Luka 12 in Biblia ya Kiswahili