Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Hesabu 26:1-25 in Swahili (individual language)

Help us?

Hesabu 26:1-25 in Biblia ya Kiswahili

1 Ilitokea baada ya tauni ambayo BWANA alimwambia Musa na Eliazari mwana wa Haruni kuhani, Alisema,
2 Wahesabu watu wote wa Israeli, kuanzia miaka ishirini na zaidi, kwa jamaa ya familia zao wote ambao wanaweza kwenda kwenye vita kwa ajili ya Israeli.”
3 Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakawaambia katika uwanda wa Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko na kusema,
4 Wahesabuni watu, kuanzi umri wa miaka ishirini na zaidi kama BWANA alivyomwamuru Musa na watu wa Israeli walitoka katika nchi ya Misri.”
5 Reubeni ndiye aliyekuwa wa kwanza, Kutoka kwa mwana wake Hanoki ulitokea ukoo wa Wahanoki. Kutoka kwa Palu ulitokea ukoo wa Wapalu.
6 Kutoka Hezroni. ulitokea ukoo wa Wahezroni. Kutoka kwa Kami ulitokea ukoo wa Wakami.
7 Hizi ndizo zilikuwa koo za uzao wa Reubeni, ambzo idadi yao ilikuwa wanaume 43, 730.
8 Eliabu alikuwa mwana wa Palu.
9 Wana wa Eliabu walikuwa ni Nemueli, Dathani. na Abiramu. Hawa ni walewale Dathani na Abiramu waliomfuata Kora waliompinga Musa na Haruni na kumpinga BWANA.
10 Pale ambapo dunia ilifungua kinywa na kuwameza pamoja na Kora wakati ambapo wafuasi wa Kora walikufa. Wakati ule, moto uliteketeza wanaume 250, amboa wlikuwa ishara ya onyo.
11 Lakini uzao wa Kora haukufa.
12 Ukoo wa uzao wa Simeoni walikuwa hawa wafuatao: Kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli, kwa Jamini, ukoo wa Wajamini, kwa Jakini, ukoo wa Wajakini,
13 kwa Zera, ukoo wa Wazera, kwa Shauli, ukoo wa Washauli.
14 Hizi ndizo koo za uzao wa Simeoni, idadi yao ilikuwa wanaume 22, 200.
15 Koo za uzao wa Gadi zilikuwa hizi: Kwa Zefoni, Ukoo wa Wazefoni, kwa Hagi, ukoo wa Wahagi, kwa Shuni, ukoo wa Washuni,
16 kwa Ozini, ukoo wa Waozini, kwa Eri, ukoo wa Waeri,
17 kwa Arodi, ukoo wa Waarodi, kwa Areli, ukoo wa Waareli.
18 Hizi ndizo koo za uzao wa Gadi, idadi yao walikuwa wanaume 40, 500.
19 Wana wa Yuda walikwa Er na Onani, lakini hawa walifia katika nchi ya Kanaani.
20 Koo zingine za uzao wa Yuda zilikuwa hizi: Kwa Shela, ukoo wa Washela, kwa Perezi, ukoo wa Waperezi, na kwa Zera, ukoo wa Wazera.
21 Uzao wa Perezi walikuwa hawa: Kwa Hezroni, ukoo wa Wahezroni, kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.
22 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda, idadi yao ilikuwa wanaume 76, 500.
23 Koo za uzao wa Isakari zilikuwa hizi: Kwa Tola, ukoo wa Watola, kwa Puva, ukoo wa Wapuva,
24 kwa Jashubu, ukoo wa Wajashubu, kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.
25 Hizi ndizo zilikuwa koo za Isakari, Idadi yao ilikuwa wanaume 64, 300.
Hesabu 26 in Biblia ya Kiswahili