Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Hesabu 22:4-15 in Swahili (individual language)

Help us?

Hesabu 22:4-15 in Biblia ya Kiswahili

4 Mfalme wa Moabu akawaambia wazee wa Midiani, “Huu umati utakula kila kitu tulicho nacho na maksai hula nyasi za kondeni.” Sasa Balaki mwana wa Zippori alikuwa mfalme wa Moabu.
5 Akatuma wajumbe kwenda kwa Balamu mwana wa Beori, kule Petho ambayo iko karibu na mto Frati, katika nchi ya taifa lake na watu wake. Akamwita na kumwambia, “Tazama, Kuna taifa ambalo wamekuja hapa tokea Misiri. Wanafunika uso wa dunia na sasa wananifuatia mimi.
6 Tafadhali naomba uje unilaanie hili taifa, kwa sababu wana nguvu kuliko mimi. Labda nitaweza kuwavamia na kuwafukuza watoke katika nchi yangu. Najua kuwa yeyote unayembariki hubarikiwa na yeyote unayemlaani atalaaniwa.”
7 Kwa hiyo wazee wa Moabu na wale wa Midiani wakaondoka, pamoja nao wakachukua malipo ya uganga. Wakafika kwa Balaamu wakamwambia maneno ya Balaki.
8 Balaamu akawaambia, “Bakini hapa usiku wa leo. Kesho nitawaletea atakachoniambia BWANA.” Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakabaki na Balaamu kwa usiku huo.
9 Mungu akaja kwa Balaamu na kumwambia, “Ni akina nani hawa waliokuja kwako?”
10 Balaamu akamjibu Mungu, “Balaki mwana wa Zippori, Mfalme wa Moabu amewatuma kwangu. Alisema,
11 'Tazama hawa watu waliotoka Misri wanafunika uso wa nchi yangu. Sasa naomba uje unilaanie hawa watu. Labada nitaweza kuwa kuwashinda na kuwafukuza.'”
12 Mungu akamjiu Balaam, “Usiambatane na hao wanaume. Na usiwalaani hawa wana wa Israeli kwa sababu wamebarikiwa.”
13 Balaamu akaamka asubuhi na kuwaambia wale viongozi wa Balaki,. “Rudini nchini kwenu kwa sababu BWANA amenikataza kuambatana nanyi.”
14 Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakaondoka na kurudi kwa Balaki. Wakamwambia, “Balaamu amekataa kuambatana nasi.”
15 Balaki akatuma viongozi wengine waliokuwa wanaheshimiwa zaidi kuliko kundi lile la awali.
Hesabu 22 in Biblia ya Kiswahili