Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 22

Hesabu 22:4-15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Mfalme wa Moabu akawaambia wazee wa Midiani, “Huu umati utakula kila kitu tulicho nacho na maksai hula nyasi za kondeni.” Sasa Balaki mwana wa Zippori alikuwa mfalme wa Moabu.
5Akatuma wajumbe kwenda kwa Balamu mwana wa Beori, kule Petho ambayo iko karibu na mto Frati, katika nchi ya taifa lake na watu wake. Akamwita na kumwambia, “Tazama, Kuna taifa ambalo wamekuja hapa tokea Misiri. Wanafunika uso wa dunia na sasa wananifuatia mimi.
6Tafadhali naomba uje unilaanie hili taifa, kwa sababu wana nguvu kuliko mimi. Labda nitaweza kuwavamia na kuwafukuza watoke katika nchi yangu. Najua kuwa yeyote unayembariki hubarikiwa na yeyote unayemlaani atalaaniwa.”
7Kwa hiyo wazee wa Moabu na wale wa Midiani wakaondoka, pamoja nao wakachukua malipo ya uganga. Wakafika kwa Balaamu wakamwambia maneno ya Balaki.
8Balaamu akawaambia, “Bakini hapa usiku wa leo. Kesho nitawaletea atakachoniambia BWANA.” Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakabaki na Balaamu kwa usiku huo.
9Mungu akaja kwa Balaamu na kumwambia, “Ni akina nani hawa waliokuja kwako?”
10Balaamu akamjibu Mungu, “Balaki mwana wa Zippori, Mfalme wa Moabu amewatuma kwangu. Alisema,
11'Tazama hawa watu waliotoka Misri wanafunika uso wa nchi yangu. Sasa naomba uje unilaanie hawa watu. Labada nitaweza kuwa kuwashinda na kuwafukuza.'”
12Mungu akamjiu Balaam, “Usiambatane na hao wanaume. Na usiwalaani hawa wana wa Israeli kwa sababu wamebarikiwa.”
13Balaamu akaamka asubuhi na kuwaambia wale viongozi wa Balaki,. “Rudini nchini kwenu kwa sababu BWANA amenikataza kuambatana nanyi.”
14Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakaondoka na kurudi kwa Balaki. Wakamwambia, “Balaamu amekataa kuambatana nasi.”
15Balaki akatuma viongozi wengine waliokuwa wanaheshimiwa zaidi kuliko kundi lile la awali.

Read Hesabu 22Hesabu 22
Compare Hesabu 22:4-15Hesabu 22:4-15