Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Hesabu 11:2-9 in Swahili (individual language)

Help us?

Hesabu 11:2-9 in Biblia ya Kiswahili

2 Ndipo watu wakamwita Musa kwa nguvu, Naye Musa akamwomba BWANA, na ule moto ukazimika.
3 Mahali pale paliitwa Tabera, kwa sababu moto wa BWANA uliwaka kati yao.
4 Baadhi ya wageni wakaanza kuweka kambi zao pamoja na wana wa wa Israeli. Walitaka kula chakula kizuri. Kisha wana wa Israeli walipoanza kulia wakisema, “Ni nani atakayetupatia nyama za kula?
5 Tunakumbuka samaki tulizokula bure kule Misri, yale matango, na matikiti maji, na mboga na vitunguu na vitunguu saumu.
6 Na sasa hatuna hamu ya kula, kwa sababu tunaona mana tu.
7 Mana ilifanana na punje ya mtama. ilionekana kama bedola.
8 watu wakazunguka kisha wakakusanyika. Wakaisaga, wakaitwanga kwa vinu, wakaitokosa nyunguni, na kuitengeneza mikate. radha yake ilikuwa kama mafuta mapya ya mizeituni.
9 Na umande ulipoanguka kambini usiku ule, na mana ilianguka pia.
Hesabu 11 in Biblia ya Kiswahili