Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Yohana 1

1Yohana 1 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Watoto wangu wapendwa, nawaandikia mambo haya kwenu ili msitende dhambi. Lakini kama mmoja wenu akitenda dhambi, tunaye wakili aliye pamoja na Baba, Yesu Kristo- ambaye ni mwenye haki.
2Yeye ni mpatanishi kwa dhambi zetu, na si kwa dhambi zetu pekee, lakini pia kwa ulimwengu mzima.
3Kwa hili twajua kwamba twamjua yeye, kama tukizitunza amri zake.
4Yeye asemaye, “Namjua Mungu,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.
5Lakini yeyote ashikaye neno lake, kweli katika mtu yule upendo wa Mungu umekamilishwa. Katika hili twajua kwamba tuko ndani yake.
6Yeye asemaye anaishi ndani ya Mungu anapaswa mwenyewe pia kuenenda kama vile Yesu Kristo alivyoenenda.
7Wapenzi, siwaandikii ninyi amri mpya, bali amri ya zamani ambayo mmekwisha kuwa nayo tangu mwanzo. Amri ya zamani ni neno ambalo mlilolisikia.
8Hata hivyo ninawaandikia ninyi amri mpya, ambayo ni kweli katika Kristo na kwenu, kwa sababu giza linapita, na nuru ya kweli iko tayari inaangaza
9Yeye asemeye yuko kwenye nuru na amchukia ndugu yake yuko katika giza hata sasa.
10Yeye ampendaye ndugu yake anaishi katika nuru na hakuna jambo lolote liwezalo kumkwaza.
11Lakini yeye amchukiaye ndugu yake yuko gizani na anatembea gizani; Yeye hajui wapi aendako, kwa sababu giza limeyapofusha macho yake.
12Nawaandikia ninyi, watoto wapendwa, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu kwa ajili ya jina lake.
13Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mnamjua Baba.
14Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mko imara, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.
15Msiipende dunia wala mambo ambayo yaliyo katika dunia. Iwapo yule ataipenda dunia, upendo wa kumpenda Baba haumo ndani yake.
16Kwani kila kitu kilichomo katika dunia- tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima- havitokani na Baba lakini vinatokana na dunia.
17Dunia na tamaa zake zinapita. Bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu huyo adumu milele.
18Watoto wadogo, ni wakati wa mwisho. Kama ambavyo mmesikia kwamba mpinga kristo anakuja, hata sasa wapinga kristo wamekuja, kwa hali hii tunajua kwamba ni wakati wa mwisho.

19Walikwenda zao kutoka kwetu, kwani hawakuwa wa kwetu. Kama vile wangekuwa wa kwetu wangeendelea kuwa pamoja nasi. Lakini wakati walipo kwenda zao, hicho kilionyesha hawakuwa wa kwetu.
20Lakini mumetiwa mafuta na yule Mtakatifu, nanyi nyote mnaijua kweli.
21Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua na kwa sababu hakuna uongo wa ile kweli
22Nani ni mwongo bali ni yeye anayepinga kwamba Yesu ni Kristo? Huyu mtu ni mpinga kristo, pale anapo mpinga Baba na Mwana.
23Hakuna anaye mpinga Mwana akawa na Baba. Yeyote anaye mkiri Mwana anaye Baba pia.
24Kama kwa ajili yenu, kile mlichosikia toka mwanzo acha kiendelee kuwa ndani yenu. Kama kile mlichosikia toka mwanzo kitakaa ndani yenu, pia, mtakaa ndani ya Mwana na Baba.
25Na hii ni ahadi aliyotupatia sisi: uzima wa milele.
26Nimewaandikia haya ninyi kuhusu wale ambao wangewaongoza ninyi katika upotevu.
27Na kwa ajili yenu, yale mafuta mliyoyapokea kutoka kwake yanakaa ndani yenu, na hamtahitaji mtu yeyote kuwafundisha. bali kama mafuta yake yanawafundisha kuhusu mambo yote na ni kweli na siyo uongo, na hata kama yameshawafundisha, kaeni ndani yake.
28Na sasa, watoto wapendwa, kaeni ndani yake, ili wakati atakapotokea, tuweze kuwa na ujasiri na siyo kujisikia aibu mbele yake katika kuja kwake.
29Kama mnajua kuwa yeye ni mwenye haki, mnajua kwamba kila mmoja atendaye haki amezaliwa na yeye.