Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Timotheo

1Timotheo 5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Usimkemee mwanamume mzee. Bali mtiye moyo kama baba yako. Uwatiye moyo vijana wa kiume kana kwamba ni ndugu zako.
2Uwatiye moyo wanawake wazee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako kwa usafi wote.
3Waheshimu wajane, wale walio wajane kweli kweli.
4Lakini kama mjane ana watoto au wajukuu, waache kwanza wajifunze kuonesha heshima kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe. Waache wawalipe wazazi wao mema, kwa kuwa hii inapendeza mbele za Mungu.
5Lakini mjane kweli kweli ni yule aliyeachwa peke yake. Naye huweka tegemeo lake kwa Mungu. Siku zote hudumu katika sala na maombi usiku na mchana.
6Hata hivyo, mwanamke yule aishiye kwa anasa amekufa, ingawaje yu hai.
7Na uyahubiri haya mambo ili kwamba wasiwe na lawama.
8Ila kama mtu asipowatunza ndugu zake, hususani wale walioko nyumbani mwake, ameikana imani na ni mmbaya kuliko mtu asiye amini.
9Basi mwanamke aandikishwe kwenye orodha kama mjane akiwa na umri usiopungua miaka sitini, na ni mke wa mume mmoja.
10Lazima awe amejulikana kwa matendo mema, ikiwa ni kwamba amewajali watoto, au ameshakuwa mkarimu kwa wageni, au ameosha miguu ya waaminio, au alimesaidia ambao wamekuwa wakiteswa, au alijitoa kwa kazi yeyote njema.
11Lakini kwa wale wajane vijana, kataa kuwaandikisha kwenye orodha ya wajane. Kwa kuwa wakiingia kwenye matamanio ya kimwili dhidi ya Kristo, wanataka kuolewa.
12Kwa njia hii huingia kwenye hatia kwa kuwa huvunja kujitoa kwao kwa awali.
13Na pia huingia kwenye mazoea ya uvivu. Wao huzunguka nyumba kwa nyumba. Si tu kwamba ni wavivu, bali pia huwa wasengenyaji na na wenye kuingilia mambo ya wengine. Wao husema mambo wasiyopaswa kuyasema.
14Kwa hiyo mimi nataka wanawake vijana waolewe, wazae watoto, wasimamie nyumba zao, ili kutokumpa adui nafasi ya kutushitaki kwa kufanya dhambi.
15Kwa sababu baadhi yao wameshamgeukia Shetani.
16Kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane, basi na awasaidie, ili kanisa lisilemewe, ili liweze kuwasaidia wale walio wajane kweli kweli.
17Basi wazee wale watawalao vyema wahesabiwe kuwa wamestahili heshima maradufu, hasa wale wanaojishughulisha na kufundisha neno la Mungu.
18Kwa kuwa maandiko yanasema, “Usimfumbe ng'ombe kinywa apulapo nafaka,” na “Mfanya kazi anastahili mshahara wake.”

19Usipokee mashitaka dhidi ya mzee isipokuwa kuna mashahidi wawili au watatu.
20Waonye wakosaji mbele ya watu wote ili wengine waliobaki labda wataogopa.
21Nakuagiza kwa dhati mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu, na malaika wateule, kwamba uzitunze maagizo haya bila ubaguzi wowote, na kwamba usifanye jambo lolote kwa upendeleo.
22Usimwekee mtu yeyote mikono haraka. Usishiriki dhambi ya mtu mwingine. Yakupasa kujitunza mwenyewe uwe usafi.
23Hakupasi kunywa maji pekee. Badala yake, unywe mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo na magonjwa yako ya mara kwa mara.
24Dhambi za baadhi ya watu hujulikana kwa uwazi, na huwatangulia hukumuni. Lakini baadhi ya dhambi hufuata baadaye.
25Vivyo hivyo, baadhi ya kazi njema hujulikana kwa uwazi, lakini hata zingine hazitafichika.