Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 89:5-18 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 89:5-18 in Biblia ya Kiswahili

5 Mbingu husifu maajabu yako, Yahwe; kweli yako inasifiwa katika kusanyiko la watakatifu.
6 Maana ni nani katika mbingu aweza kulinganishwa na Yahwe? Ambaye kati ya wana wa miungu ni kama Yahwe?
7 Ni Mungu anaye heshimiwa sana katika baraza la watakatifu naye ni wakutisha kati ya wote wanao mzunguka.
8 Yahwe, Mungu wa majeshi, ni nani aliye na nguvu kama wewe, Yahwe? Kweli yako inakuzunguka.
9 Wewe huitawala bahari yenye nguvu; mawimbi yainukapo, wewe huyatuliza.
10 Ulimwangamiza Rahabu kama mmoja aliye uliwa. Uliwatawanya adui zako kwa mkono wako wenye nguvu.
11 Mbingu ni zako wewe, na nchi pia. Uliiumba dunia na vyote vilivyomo.
12 Uliumba kaskazini na kusini. Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
13 una mkono wa uweza na mkono wenye nguvu, na mkono wako wa kuume uko juu.
14 Haki na hukumu ni msingi wa kiti chako. Uaminifu wa agano lako na uaminifu huja mbele zako.
15 Wamebarikiwa watu wakuabuduo wewe! Yahwe, wanatembea katika nuru ya uso wako.
16 Siku zote wanafurahia katika jina lako, na katika haki yako wanakutukuza wewe.
17 Wewe ni fahari ya nguvu zao, na kwa nguvu zako tu washindi.
18 Maana ngao zetu ni za kwako Yahwe; mfalme wetu ni wa Mtakatifu wa Israeli.
Zaburi 89 in Biblia ya Kiswahili