Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 89:36-50 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 89:36-50 in Biblia ya Kiswahili

36 uzao wake utaendelea milele na kiti chake cha enzi kama vile jua mbele yangu.
37 Kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu mawinguni.” Selah
38 Lakini wewe umemtupa na kumkataa; umemkasirikia mfalme mpakwa mafuta wako.
39 Wewe umelikataa agano la mtumishi wako. Umeinajisi taji yake ardhini.
40 Umevunja kuta zake zote. Umeharibu ngome yake.
41 Wapita njia wote wamemuibia, amekuwa kitu chenye kinyaa kwa majirani zake.
42 Umeinua mkono wa kuume wa adui zake; umewafurahisha adui zake wote.
43 Umeyageuza makali ya upanga wake. Na hukumfanya asimame awapo vitani.
44 Umeimaliza fahari yake; umekitupa ardhini kiti chake cha enzi.
45 Umefupisha siku za ujana wake. Umemfunika kwa aibu. Selah
46 Mpaka lini, Yahwe? utajificha, milele? Mpaka lini hasira yako itawaka kama moto?
47 Oh, fikiria jinsi muda wangu ulivyo mfupi, na ni kwa ajili gani umewaumba wana wote wa wanadamu wasio na manufaa!
48 Ni nani aweza kuishi na asife, au atakaye iokoa nafsi yake dhidi ya mkono wa kuzimu? Selah
49 Bwana, yako wapi matendo yako ya zamani ya uaminifu wa agano ambayo ulimwapia Daudi katika kweli yako?
50 Kumbuka, Bwana, watumishi wako walivyodhihakiwa na vile nilivyo vumilia moyoni mwangu matusi mengi dhidi ya mataifa.
Zaburi 89 in Biblia ya Kiswahili