Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 71:4-13 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 71:4-13 in Biblia ya Kiswahili

4 Uniokoe mimi, Mungu wangu, kutoka katika mkono wa asiye haki na katili.
5 Maana wewe ni tumaini langu, Bwana Yahwe. Nimekuamini wewe siku zote tangu nilipokuwa mtoto.
6 Nimekuwa nikisaidiwa na wewe tangu tumboni; wewe ndiye yule uliyenitoa tumboni mwa mama yangu; sifa zangu zitakuhusu wewe siku zote.
7 Mimi ni mfano bora kwa watu wangu; wewe ni kimbilio langu lenye nguvu.
8 Mama yangu atajawa na sifa zako, siku zote akikuheshimu.
9 Usinitupe katika siku za miaka ya uzee wangu; usiniache wakati nguvu zangu zitakapoisha.
10 Maana adui zangu wanazungumza kuhusu mimi; wale wanao fatilia uhai wangu wanapanga njama pamoja.
11 Wao husema, “Mungu amemuacha; mfuateni na mumchukue, maana hakuna yeyote awezaye kumuokoa yeye.”
12 Mungu, usiwe mbali nami; Mungu wangu, harakisha kunisaidia mimi.
13 Waaibishwe na kuharibiwa, wale walio adui wa uhai wangu; wavishwe laumu na kudharauliwa, wale watafutao kuniumiza.
Zaburi 71 in Biblia ya Kiswahili