Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 71:2-12 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 71:2-12 in Biblia ya Kiswahili

2 Uniokoe na kunifanya salama katika haki yako; geuzia sikio lako kwangu.
3 Uwe kwagu mwamba kwa ajili ya kimbilio salama ambako naweza kwenda siku zote; wewe umeamuru kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.
4 Uniokoe mimi, Mungu wangu, kutoka katika mkono wa asiye haki na katili.
5 Maana wewe ni tumaini langu, Bwana Yahwe. Nimekuamini wewe siku zote tangu nilipokuwa mtoto.
6 Nimekuwa nikisaidiwa na wewe tangu tumboni; wewe ndiye yule uliyenitoa tumboni mwa mama yangu; sifa zangu zitakuhusu wewe siku zote.
7 Mimi ni mfano bora kwa watu wangu; wewe ni kimbilio langu lenye nguvu.
8 Mama yangu atajawa na sifa zako, siku zote akikuheshimu.
9 Usinitupe katika siku za miaka ya uzee wangu; usiniache wakati nguvu zangu zitakapoisha.
10 Maana adui zangu wanazungumza kuhusu mimi; wale wanao fatilia uhai wangu wanapanga njama pamoja.
11 Wao husema, “Mungu amemuacha; mfuateni na mumchukue, maana hakuna yeyote awezaye kumuokoa yeye.”
12 Mungu, usiwe mbali nami; Mungu wangu, harakisha kunisaidia mimi.
Zaburi 71 in Biblia ya Kiswahili