Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 71:13-21 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 71:13-21 in Biblia ya Kiswahili

13 Waaibishwe na kuharibiwa, wale walio adui wa uhai wangu; wavishwe laumu na kudharauliwa, wale watafutao kuniumiza.
14 Lakini nitakutumainia wewe siku zote na nitakusifu wewe zaidi na zaidi.
15 Kinywa changu kitaongea kuhusu haki yako na wokovu wako mchana kutwa, ingawa ziwezi kuzielewa maana ni nyingi mno.
16 Nitakuja na matendo yenye nguvu ya Bwana Yahwe; nitataja haki yako, yako pekee.
17 Mungu, tangu ujana wangu wewe umenifundisha; hata sasa ninatangaza matendo yako ya ajabu.
18 Hakika, hata niwapo mzee na mvi kichwani, Mungu, usiniache mimi, kama ambavyo nimekuwa nikitanga nguvu yako kwa vizazi vijavyo, na uweza wako kwa yeyote ajaye.
19 Pia haki yako, Mungu, iko juu sana; wewe ambaye umefanya mambo makuu, Mungu, ni nani aliye kama wewe?
20 Wewe ambaye umetuonesha sisi mateso mengi utatuhuisha tena na utatupandisha tena juu kutoka kwenye kina cha nchi.
21 Uiongeze heshima yangu; rudi tena na unifariji.
Zaburi 71 in Biblia ya Kiswahili