Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 68:6-20 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 68:6-20 in Biblia ya Kiswahili

6 Mungu huwaweka wakiwa katika familia; yeye huwafungua wafungwa kwa kuimba bali waasi huishi katika ardhi kavu.
7 Mungu, wewe ulipoenda mbele ya watu wako, ulipotembea kupitia jangwani, Selah
8 nchi ilitetemeka; mbingu pia zilidondosha mvua katika uwepo wa Mungu, uweponi mwa Mungu wakati alipokuja Sinai, uweponi mwa Mungu, Mungu wa Israeli.
9 Wewe, Mungu, ulituma mvua nyingi; uliuimarisha urithi wako wakati ulipokuwa umechoka.
10 Watu wako waliishi humo; Wewe, Mungu, uliutoa kwa wema wako kwa maskini.
11 Bwana alitoa amri, na wale walio zitangaza walikuwa ni jeshi kuu.
12 Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia, na wanawake wakisubiri nyumbani kuvigawana wao na familia zao vilivyotekwa nyara.
13 Njiwa walio vikwa fedha wakiwa na mabawa ya njano ya dhahabu. Wakati baadhi ya watu wakikaa kati ya mifugo ya kondoo, kwa nini umefanya haya?
14 Mwenyezi Mungu aliwatawanya Wafalme huko, ilikuwa kama vile wakati wa theluji juu ya Mlima Salmoni.
15 Mlima mkubwa ni milima wa mji wa Bashani; mlima mrefu ni mlima wa mji wa Bashani.
16 Ewe mlima mrefu wa nchi, kwa nini unatazama kwa jicho la husuda, kwenye mlima ambao Mungu ameutaka kwa ajili ya mahali ambapo yeye ataishi? Hakika, Yahwe ataishi humo milele.
17 Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu juu ya maelfu; Bwana yu kati yao katika mahari patakatifu, kama katika Sinai.
18 Wewe umepaa juu; uliwaongoza mateka; umepokea zawadi kutoka kati ya watu, hata kutoka kwa wale waliopigana dhidi yako, ili kwamba wewe, Yahwe Mungu, uweze kuishi huko.
19 Abarikiwe Bwana, atubebeaye mizigo yetu, Mungu ambaye ni wokovu wetu. Selah
20 Mungu wetu ni Mungu aokoaye; Yahwe Bwana ni yule awezaye kutuokoa sisi dhidi ya kifo.
Zaburi 68 in Biblia ya Kiswahili