Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 66:11-18 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 66:11-18 in Biblia ya Kiswahili

11 Wewe ulituingiza sisi kwenye wavu; uliweka mzigo mzito viunoni mwetu.
12 Wewe uliwafanya watu wasafiri juu ya vichwa vyetu; tulipita motoni na majini, lakini ukatuleta mahali pa wazi palipo salama.
13 Nitaingia nyumbani mwako nikiwa na sadaka ya kuteketezwa; nitakulipa viapo vyangu
14 ambavyo midomo yangu iliahidi na kinywa changu kiliongea nilipokuwa katika dhiki.
15 Nitakutolea sadaka ya kuteketezwa ya wanyama wanene pamoja na harufu nzuri ya kondoo waume; Nitatoa ng'ombe na mbuzi. Selah
16 Njoni, msikie, ninyi nyote mnao mwabudu Mungu, nami nitatangaza yale yeye aliyoitendea roho yangu.
17 Nilimlilia kwa kinywa changu, naye alipendezwa na ulimi wangu.
18 Kama ningelikuwa na dhambi ndani ya moyo wangu, Bwana asingenisikiliza.
Zaburi 66 in Biblia ya Kiswahili