Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 59:8-14 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 59:8-14 in Biblia ya Kiswahili

8 Lakini wewe, Yahwe, utawacheka; wewe huwadhihaki mataifa yote.
9 Mungu, nguvu yangu, nitakuwa msikivu kwako; wewe ni mnara wangu mrefu.
10 Mungu atakutana nami akiwa na uaminifu wa agano lake; Mungu atanifanya nione shauku yangu juu ya adui zangu.
11 Usiwaue, hivyo watu watasahau. Uwatawanye kwa nguvu zako na uwaangushe, Bwana ngao yetu.
12 Kwa ajili ya dhambi za midomo yao na maneno ya midomo yao, wakamatwe katika majivuno yao, na kwa laana na uongo ambao wao huelezea.
13 Uwamalize katika gadhabu yako, uwamalize ili kwamba wasiwepo tena; wajue kuwa Mungu anatawala katika Yakobo na mwisho wa nchi. Selah
14 Wakati wa jioni wao hurudi, wakibweka kama mbwa wakiuzungukia mji.
Zaburi 59 in Biblia ya Kiswahili