Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 59:3-8 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 59:3-8 in Biblia ya Kiswahili

3 Maana, tazama, wanasubiria uvamizini waniue. Wafanya maovu wenye nguvu hujikusanya wenyewe pamoja dhidi yangu, lakini sio kwa sababu ya makosa yangu au dhambi yangu, Yahwe.
4 Wao wanajiandaa kunikimbiza ingawa sina kosa; amka unisaidie na unitazame.
5 Ewe, Yahwe Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, inika uwaadhibu mataifa yote; usiwe na huruma kwa mhalifu mwovu yeyote. Selah
6 Wao wanarudi jioni, wanabweka kama mbwa na kuuzungukia mji.
7 Tazama, wanapiga kelele mbaya kwa midomo yao; panga ziko kwenye midomo yao, maana wanasema, “Ni nani anaye tusikia?”
8 Lakini wewe, Yahwe, utawacheka; wewe huwadhihaki mataifa yote.
Zaburi 59 in Biblia ya Kiswahili