Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 55:11-22 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 55:11-22 in Biblia ya Kiswahili

11 Uovu uko katikati yake; ukandamizaji na uongo hauiachi mitaa yake.
12 Kwa maana hakuwa adui aliye nikemea, hivyo ningevumilia; wala ingekuwa ni yule aliye nichukia aliyejiinua mwenyewe dhidi yagu, hivyo ningejificha asinione.
13 Lakini ulikuwa wewe, mtu sawa na mimi, mwenzangu na rafiki yangu.
14 Tulikuwa na ushirika mtamu pamoja; tuliingia katika nyumba ya Mungu tukiwa na umati mkubwa.
15 Kifo na kiwapate ghafla; na washuke wakiwa hai kuzimuni, maana ndiko waishiko waovu, hapo hapo kati yao.
16 Lakini kwangu mimi, nitamwita Mungu, na Yahwe ataniokoa.
17 Wakati wa jioni, asubuhi na mchana ninalalamika na kuomboleza; yeye atasikia sauti yangu.
18 Kwa usalama kabisa atayaokoa maisha yangu na vita dhidi yangu, kwa maana wale waliopigana nami walikuwa ni wengi.
19 Mungu, yule unayetawala milele, atawasikia na kuwaaibisha wao. Selah Hawabadiliki, na hawamhofu Mungu.
20 Rafiki yangu ameinua mikono yake dhidi ya wale waliokuwa na amani naye; Hakuheshimu agano alilokuwa nalo.
21 Mdomo wake ulikuwa laini kama siagi, lakini moyo wake ulikuwa adui; maneno yake yalikuwa laini kuliko mafuta, lakini yalikuwa ni panga zilizochomolewa.
22 Umtwike mizigo yako Yahwe, naye atakusaidia; yeye hataruhusu mtu mwenye haki kuyumbayumba.
Zaburi 55 in Biblia ya Kiswahili