1 Uyategee sikio maombi yangu, Mungu; nawe usijifiche mbali na kusihi kwangu.
2 Unitazame kwa makini na unijibu; Sina pumziko katika shida zangu
3 kwa sababu ya sauti ya adui zangu, kwa sababu ya ukandamizaji wa waovu; maana wananiletea matatizo na kunitesa wakiwa na hasira.
4 Moyo wangu wasumbuka ndani yangu, na hofu ya kifo imeniangukia.
5 Uwoga na kutetemeka kumenijia, nayo hofu imenielemea.
6 Nikasema, “Oh, kama tu ningekuwa na mabawa kama njiwa! Ningelipaa mbali na kupata pumziko.
7 Tazama, ningeenda mbali; ningekaa jangwani. Selah
8 Ningefanya haraka kuja mafichoni mwako kuzikimbia dhoruba na tufani.”
9 Uwaangamize, Bwana, vuruga lugha zao! Kwa maana nimeona vurugu na ugomvi katika mji.
10 Mchana na usiku wao huenda kwenye kuta zake; uchafu na ufisadi uko katikati yake.
11 Uovu uko katikati yake; ukandamizaji na uongo hauiachi mitaa yake.