Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 49:7-15 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 49:7-15 in Biblia ya Kiswahili

7 Ni hakika kuwa hakuna yeyote atakaye muokoa ndugu yake au kumpa Mungu pesa kwa ajili yake,
8 Kwa maana ukombozi wa uhai wa mtu ni gharama kubwa, na hakuna awezaye kulipa kile tunacho daiwa.
9 Hakuna yeyote atakaye ishi milele ili mwili wake usioze.
10 Maana yeye ataona uozo. Watu wenye hekima hufa; wajinga pia huangamia na kuacha mali zao kwa wengine.
11 Mawazo yao ya ndani ni kuwa familia zao zitaishi milele, na mahali waishipo, kwa vizazi vyote; wanaita ardhi zao kwa majina yao wenyewe.
12 Lakini mtu, kuwa na mali, haimaanishi atabaki hai; kama wanyama walioangamia.
13 Hii ni hatma ya wafanyao ujinga baada ya kufa,...
14 Kama kondoo wamechaguliwa kwa ajili ya kuzimu na kifo kitakuwa mchungaji wao. Nao watatawaliwa na wenye haki ifikapo asubuhi, na miili yao italiwa kuzimuni, wakiwa hawana afasi ya kuishi kwa ajili yao.
15 Bali Mungu ataufufua uhai wangu kutoka katika nguvu ya kuzimu; naye atanipokea. Selah
Zaburi 49 in Biblia ya Kiswahili