6 Kwa maana sitauamini upinde wangu, wala upanga wangu hautaniokoa.
7 Bali wewe ndeye uliyetuokoa na adui zetu, na umewaaibisha wale watuchukiao.
8 Katika Mungu tumefanywa kujivuna siku zote, nasi tutalishukuru jina lako milele. Selah
9 Lakini sasa umetutupa na kutufedhehesha, na hauendi na majeshi yetu.
10 Umetufanya kuwakimbia maadui zetu; na wale watuchukiao huchukua vitu vyetu vya thamani kwa ajili yao wenyewe.
11 Umetufanya kama kondoo aliyeandaliwa kwa ajili ya chakula na umetutawanya kati ya mataifa.
12 Wewe unawauza watu wako bure; kwa kufanya hivyo haukupata faida.
13 Wewe umetufanya kukemewa na majirani zetu, kuchekwa, na kudhihakiwa na wale wanao tuzunguka.
14 Umetufaya kituko kati ya mataifa,...
15 Siku zote fedheha yangu iko mbele yangu, na aibu ya uso wangu imenifunika
16 kwa sababu ya sauti yake iliyo kemea na kutukana, kwa sababu ya adui na kisasi.
17 Yote haya yametupata sisi; bado hatukukusahau wewe wala kulikosea agano lako.