Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 37:8-27 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 37:8-27 in Biblia ya Kiswahili

8 Usikasilile na kugadhabika. Usiogope. Hii huleta matatizo tu.
9 Watendao maovu watafutiliwa mbali, bali wale wamngojao Yahwe watairithi nchi.
10 Katika muda mfupi mtu mwovu atatoweka; wewe utatazama mahali pake, wala hautamuona.
11 Lakini wapole watairithi nchi nao watafurahia katika mafanikio makubwa.
12 Mtu mwovu hupanga njama kinyume na mwenye haki na kumsagia meno.
13 Bwana humcheka, kwa maana anaona siku yake inakuja.
14 Waovu wametoa nje panga zao na wametayarisha pinde zao ili kuwaangamiza wanyonge na wahitaji, na kuwaua wenye haki.
15 Panga zao zitawaua wenyewe, na pinde zao zitavunjika.
16 Ni bora kuwa mwenye haki maskini kuliko tajiri mwenye mali nyingi.
17 Kwa maana mikono ya watu waovu itavunjika, bali Yahwe huwasaidia watu wenye haki.
18 Yahwe huwalinda watu wasio na lawama siku hadi siku, na urithi wao utakuwa wa milele.
19 Hawata aibika siku mbaya zijapo. Wakati wa njaa ufikapo wao watakuwa na chakula cha kutosha.
20 Bali waovu wataangamia. Maadui wa Yahwe watakuwa kama vile utukufu wa malisho; watamalizwa na kupotezwa katika moshi.
21 Mtu mwovu hukopa lakini halipi, bali mtu mwenye haki ni mkarimu na hutoa.
22 Wale walio barikiwa na Mungu watairithi nchi; wale aliowalaani watafutiliwa mbali.
23 Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu.
24 Ajapojikwaa, hataanguka chini, kwa kuwa Yahwe anamshikilia kwa mkono wake.
25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; sijawahi kumuona mtu mwenye haki ametelekezwa wala watoto wake kuombaomba mkate.
26 Wakati wote yeye ni mkarimu na hukopesha, nao watoto wake hufanyika baraka.
27 Acha uovu na ufanye yaliyo mema; ndipo utakapokuwa salama milele.
Zaburi 37 in Biblia ya Kiswahili