Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 31:7-23 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 31:7-23 in Biblia ya Kiswahili

7 Nitafurahi na kushangilia katika uaminifu wa agano lako, kwa kuwa uliyaona mateso yangu; wewe uliijua dhiki ya moyo wangu.
8 Wewe haujaniweka kwenye mkono wa maadui zangu. Nawe umeiweka miguu yangu mahali pa wazi papana.
9 Uniurumie, Yahwe, kwa maana niko katika dhiki; macho yangu yanafifia kwa huzuni pamoja na moyo wangu na mwili wangu.
10 Kwa kuwa maisha yangu yamechoshwa kwa huzuni na miaka yangu kwa kuugua kwangu. Nimekuwa dhaifu kwa sababu ya dhambi zangu, na mifupa yangu inachakaa.
11 Kwa sababu ya maadui zangu wote, watu wananibeza; majirani zangu wanaishangaa hali yangu, na wale wanao nifahamu wanashtuka. Wale wanionao mitaani hunikimbia.
12 Nimesahaulika kama mtu aliye kufa ambaye hakuna mtu anaye mfikiria. Niko kama chungu kilicho pasuka.
13 Kwa maana nimesikia minong'ono ya wengi, habari za kutisha kutoka pande zote kwa pamoja wamepanga njama kinyume na mimi. Wao wanapanga njama ya kuniua.
14 Bali mimi ninakuamini wewe, Yahwe; Ninasema, “Wewe ni Mungu wangu.”
15 Hatima yangu iko mikononi mwako. Uniokoe mikononi mwa maadui zangu na wale wanao nifukuzia.
16 Nuru ya uso wako imuangazie mtumishi wako; uniokoe katika uaminifu wa agano lako.
17 Usiniache niaibishwe, Yahwe; kwa maana ninakuita wewe! Waovu waaibishwe! Na wanyamaze kimya kuzimuni.
18 Na inyamazishwe midomo midanganyifu ambayo husema maneno mabaya kuhusu watu wenye haki huku wakiwa na kiburi na dharau.
19 Uzuri wako ni wa namna gani nao umeuhifadhii kwa ajili ya wale wanao kuheshimu sana, ambao wewe huufanya kwa ajili ya wale ambao hukimbilia kwako kwa ajili ya usalama mbele ya watoto wote wa wanadamu!
20 Katika makao ya uwepo wako, wewe huwaficha mbali na njama za watu. Wewe huwaficha mahali salama na ndimi zenye vurugu.
21 Atukuzwe Yahwe, kwa maana yeye alinionesha maajabu ya uaminifu wa agano lake mahali nilipoishi.
22 Ingawa kwa haraka zangu nilisema, “Nimeondolewa machoni pako,” bali wewe ulisikia kusihi kwangu nilipokulilia wewe.
23 Enyi wafuasi waaminifu, mpendeni Yahwe, Yahwe huwalinda waaminifu, lakini huwalipa wakaidi ipasavyo.
Zaburi 31 in Biblia ya Kiswahili