10 Kwa kuwa maisha yangu yamechoshwa kwa huzuni na miaka yangu kwa kuugua kwangu. Nimekuwa dhaifu kwa sababu ya dhambi zangu, na mifupa yangu inachakaa.
11 Kwa sababu ya maadui zangu wote, watu wananibeza; majirani zangu wanaishangaa hali yangu, na wale wanao nifahamu wanashtuka. Wale wanionao mitaani hunikimbia.
12 Nimesahaulika kama mtu aliye kufa ambaye hakuna mtu anaye mfikiria. Niko kama chungu kilicho pasuka.
13 Kwa maana nimesikia minong'ono ya wengi, habari za kutisha kutoka pande zote kwa pamoja wamepanga njama kinyume na mimi. Wao wanapanga njama ya kuniua.
14 Bali mimi ninakuamini wewe, Yahwe; Ninasema, “Wewe ni Mungu wangu.”
15 Hatima yangu iko mikononi mwako. Uniokoe mikononi mwa maadui zangu na wale wanao nifukuzia.