Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 31:1-12 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 31:1-12 in Biblia ya Kiswahili

1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. In wewe, Yahwe, nakimbilia usalama; usiniache niaibishwe. Katika haki yako uniokoe.
2 Unisikie; uniokoe haraka; uwe mwamba wangu wa usalama, ngome ya kuniokoa.
3 Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu; kwa hiyo kwa ajili ya jina lako, uniongoze na unielekeze.
4 Unitoe katika mtego ambao wameuficha kwa ajili yangu, kwa kuwa wewe ni usalama wangu.
5 Mikononi mwako naikabidhi roho yangu; nawe utaniokoa, Yahwe, mwenye kuaminika.
6 Ninawachukia wale wanaotumikia miungu isiyo na maana, bali ninaamini katika Yahwe.
7 Nitafurahi na kushangilia katika uaminifu wa agano lako, kwa kuwa uliyaona mateso yangu; wewe uliijua dhiki ya moyo wangu.
8 Wewe haujaniweka kwenye mkono wa maadui zangu. Nawe umeiweka miguu yangu mahali pa wazi papana.
9 Uniurumie, Yahwe, kwa maana niko katika dhiki; macho yangu yanafifia kwa huzuni pamoja na moyo wangu na mwili wangu.
10 Kwa kuwa maisha yangu yamechoshwa kwa huzuni na miaka yangu kwa kuugua kwangu. Nimekuwa dhaifu kwa sababu ya dhambi zangu, na mifupa yangu inachakaa.
11 Kwa sababu ya maadui zangu wote, watu wananibeza; majirani zangu wanaishangaa hali yangu, na wale wanao nifahamu wanashtuka. Wale wanionao mitaani hunikimbia.
12 Nimesahaulika kama mtu aliye kufa ambaye hakuna mtu anaye mfikiria. Niko kama chungu kilicho pasuka.
Zaburi 31 in Biblia ya Kiswahili