Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 22:12-27 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 22:12-27 in Biblia ya Kiswahili

12 Maksai wengi wananizunguka mimi; maksai wenye nguvu ya Bashan wananizunguka mimi.
13 Wao wanafungua midomo yao kwangu kama simba aungurumaye akirarua windo lake.
14 Ninamwagwa nje kama maji, na mifupa yangu yote imeteguka. Moyo wangu ni kama nta; nao unayeyuka ndani ya sehemu zangu za ndani.
15 Nguvu zangu zimekaushwa kama kipande cha ufinyanzi; ulimi wangu unanata juu ya mdomo wangu. Wewe umenilaza mimi katika vumbi la mauti.
16 Kwa maana mbwa wamenizunguka; kundi la watu waovu limenizunguka; wamenitoboa mikono yangu na miguu yangu.
17 Nami ninaweza kuihesabu mifupa yangu. Wao wananitazama na kunishangaa.
18 Wao wanagawa mavazi yangu kati yao wenyewe, wanapiga kura kwa ajili ya mavazi yangu.
19 Usiwe mbali, Yahwe; tafadhali harakisha kunisaidia mimi, nguvu yangu!
20 Uiokoe roho yangu na upanga, maisha yangu mwenyewe na makucha ya mbwa mwitu.
21 Uniokoe na mdomo wa simba; uniokoe na mapembe ya ng'ombe wa porini.
22 Nami nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu; katikati ya kusanyiko la watu nitakusifu wewe.
23 Ninyi mnao mwogopa Yahwe, msifuni yeye! Ninyi nyote kizazi cha Yakobo, muheshimuni yeye! Simameni katika hofu yake, ninyi nyote kizazi cha Israeli!
24 Kwa kuwa haja dharau au kuchukia mateso ya aliye taabishwa; Yahwe hajamficha uso wake yeye; pindi wale walio taabishwa walipo mlilia yeye, yeye alisikia.
25 Yahwe, katika kusanyiko la watu wako nitakusifu kwa yale uliyo tenda; nami nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wanao muhofu yeye.
26 Walio onewa watakula na kutosheka; wale ambao humtafuta Yahwe watamsifu yeye. Mioyo yenu iishi milele.
27 Watu wote wa duniani watakumbuka na kumrudia Yahwe; familia zote za mataifa watapiga magoti chini mbele yako.
Zaburi 22 in Biblia ya Kiswahili