1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mfalme anashangilia katika uweza wako, Yahwe! Ni kwa namna kuu anashangilia katika wokovu uliouleta!
2 Wewe umempa yeye matamanio ya moyo wake na hauja mkatalia maombi midomo yake.
3 Kwa kuwa wewe unamletea baraka nyingi; wewe uliweka katika kichwa chake taji ya dhahabu iliyo safi kabisa.
4 Yeye alikuomba wewe maisha; ukampatia maisha; wewe ulimpatia maisha malefu milele na milele.
5 Yeye utukufu wake ni mkuu kwa sababu ya ushindi wako; wewe umemuwekea mapambo na enzi.
6 Kwa kuwa unampatia yeye baraka za kudumu; unamfurahisha kwa furaha ya uwepo wako.
7 Kwa kuwa Mfalme humwamini Yahwe; kwa kupitia uaminifu wa agano la aliye juu zaidi yeye hataondolewa.
8 Mkono wako utawakamata adui zangu wote wote; mkono wako wa kuume utawakamata wale wote wanao kuchukia.
9 Wakati wa hasira yako, wewe utawachoma kama katika tanuru la moto. Yahwe atawamaliza wao katika hasira yake, na moto utawateketeza upesi wao.