Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 135:3-8 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 135:3-8 in Biblia ya Kiswahili

3 Msifuni Yahwe, kwa kuwa ni mwema; liimbieni sifa jina lake, maana ni vizuri kufanya hivyo.
4 Kwa kuwa Yahwe amemchagua Yakobo kwa ajili yake mwenyewe, Israeli kama urithi wake.
5 Najua ya kuwa Yahwe ni mkuu, na kwamba Bwana wetu yuko juu ya miungu yote.
6 Chochote Yahwe apendacho, hufanya mbinguni, duniani, katika bahari na katika vilindi vyote.
7 Hushusha mawingu kutoka mbali, akifanya mianga ya radi kuongozana na mvua na kuleta upepo toka katika ghala yake.
8 Aliua mzaliwa wa kwanza wa Misri, wote wanadamu na wanyama.
Zaburi 135 in Biblia ya Kiswahili