Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 119:82-124 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 119:82-124 in Biblia ya Kiswahili

82 Macho yangu yanatamani sana kuiona ahadi yako; ni lini utanifariji mimi?
83 Kwa maana nimekuwa kama kiriba katika moshi; sisahau sheria zako.
84 Ni kwa muda gani gani mtumishi wako atalazimika kuyavumilia haya; ni lini utawahukumu wale wanaonitesa?
85 Wenye kiburi wamenichimbia shimo, wasiotii sheria yako.
86 Amri zako zote ni za kuaminika; wale watu walinitesa bila ya haki; unisaidie.
87 karibu kunifanya nifikie mwisho juu ya nchi hii, lakini siyakatai maagizo yako.
88 Kwa upendo wako thabiti, uniweke hai, ili niweze kuzitii amri zako. LAMEDH.
89 Yahwe, neno lako linasimama milele; neno lako limefanywa imara mbinguni.
90 Uaminifu wako wadumu kwa ajili ya vizazi vyote; umeiimarisha nchi, nayo inadumu.
91 Vitu yote yaliendelea mpaka leo hii, kama vile ulivyosema katika amri zako za haki, maana vitu vyote ni watumishi wako.
92 Kama sheria yako isingekuwa furaha yangu, ningeangamia katika mateso yangu.
93 Sitayasahau kamwe maagizo yako, maana kupitia hayo umeniweka hai.
94 Mimi ni wako, kwa maana ninayatafuta maagizo yao.
95 Waovu hujiandaa kuniangamiza, lakini nitatafuta kuzielewa amri za agano lako.
96 Nimeona kuwa kila kitu kina mipaka, lakini amri zako ni pana, zaidi ya mipaka. MEM.
97 Oh ni jinsi gani naipenda sheria yako! Ni tafakari yangu mchana kutwa.
98 Amri zako hunifanya mwenye hekima kuliko adui zangu, maana amri zako siku zote ziko pamoja nami.
99 Ninauelewa zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa maana ninazitafakari amri za agano lako.
100 Ninaelewa kuliko wale wanaonizidi umri; hii ni kwa sababu nimeyashika maagizo yako.
101 Nimeiepusha miguu yangu na kila njia ya uovu ili niweze kulitii neno lako.
102 Sijaenda kinyume na amri zako za haki, kwa maana wewe umenifundisha.
103 Ni jinsi gani maneno yako ni matamu kwenye majaribu yangu, naam, matamu kuliko asali kinywani mwangu!
104 Kupitia maagizo yako ninapata utambuzi; kwa hiyo kila njia isiyo ya kweli.
105 Neno lako ni taa ya mguu miguu yangu na mwanga wa njia yangu.
106 Nimeapa na nimethibitisha, kuwa nitazitii amri za haki yako.
107 Nimeteswa sana; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika neno lako.
108 Yahwe, tafadhali pokea dhabihu yangu ya hiari ya kinywa changu, na unifundishe amri zako za haki.
109 Uhai wangu ziku zote uko mkononi mwangu, lakini bado sisahau sheria yako.
110 Waovu wamenitegea mtego, lakini sijapotea mbali na maagizo yako.
111 Nimezifanya amri za agano lako kama urithi wangu milele, maana hizo ni furaha ya moyo wangu.
112 Moyo wangu umewekwa kuzitii sheria zako milele mpaka mwisho kabisa. SAMEKH.
113 Ninawachukia watu wa kusita-sita, lakini naipenda sheria yako.
114 Wewe ni ficho langu na ngao yangu; nalingoja neno lako.
115 Ondokeni kwangu, ninyi mtendao uovu, ili niweze kuzitii amri za Mungu wangu.
116 Uniwezeshe kwa neno lako ili niweze kuishi na nisiaibike na matumaini yangu.
117 Unisaidie, nami nitakuwa salama; siki zote nitazitafakari sheria zako.
118 Wewe huwakataa wale wote wapoteao mbali na sheria zako, maana watu hao ni wadanganyifu na si wakuaminika.
119 Wewe huwaondoa waovu wa nchi kama takataka; kwa hiyo ninazipenda amri zako thabiti.
120 Mwili wangu hutetemeka kwa hofu yako, na ninaziogopa amri za haki yako. AYIN.
121 Ninafanya kilicho sahihi na haki; usiniache kwa watesi wangu.
122 Uwe mdhamini wa ustawi wa mtumishi wako; usiwaache wenye kiburi wanionee.
123 Macho yangu yanachoka kwa kuusubiri wokovu wako na neno lako la haki.
124 Mwoneshe mtumishi wako uaminifu wa agano lako, na unifundishe sheria zako.
Zaburi 119 in Biblia ya Kiswahili