59 Nilizichunguza njia zangu na kugeuzia miguu yangu kwenye amri za agano lako.
60 Naharakisha na sichelewi kuzishika amri zako.
61 Kamba za waovu zimenifunga; nami sijaisahau sheria yako.
62 Katikati ya usiku ninaamka kukushukuru wewe kwa sababu ya amri za haki yako.
63 Ninaurafiki na wale wanao kuabudu wewe, wale wote watiio maagizo yako.
64 Yahwe, nchi, imejaa uaminifu wa agano lako; unifundishe sheria zako. TETH.
65 Wewe umemtendea mema mtumishi wako, Yahwe, sawasawa na neno lako.
66 Unifundishe utambuzi sahihi na uelewa, kwa kuwa nimeamini katika amri zako.
67 Kabla sijateswa nilipotea, lakini sasa nimelitii neno lako.
68 Wewe ni mwema, na ndiye yule utendaye mema; unifundishe sheria zako.
69 Wenye kiburi wamenichafua kwa uongo, lakini niliyashika maagizo yako kwa moyo wangu wote.
70 Mioyo yao ni migumu, lakini ninafurahia katika sheria yako.
71 Ni vizuri kwangu kuwa nimeteseka ili niweze kujifunza sheria zako.
72 Maagizo yatokayo kinywani mwako ni ya thamani zaidi kwangu kuliko maelfu ya vipande vya dhahabu na fedha. YOD.
73 Mikono yako imeniumba na kunitengeneza; unipe uelewa ili niweze kujifunza amri zako.
74 Wale wanao kucha wewe watafurahi wanionapo kwa sababu ninapata tumaini katika neno lako.
75 Ninajua, Yahwe, kuwa amri zako ni za haki, na kuwa katika uaminifu ulinitesa.
76 Agano lako aminifu na linifariji, kama ulivyomwahidi mtumishi wako.
77 Unihurumie ili niweze kuishi, kwa maana sheria yako ni furaha yangu.
78 Wenye kiburi na waaibishwe, maana wamenitukana; bali mimi nitayatafakari maagizo yako.
79 Wale wote wanao kucha wewe na wanigeukie, wale wazijuao amri za agano lako.