Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 119:34-57 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 119:34-57 in Biblia ya Kiswahili

34 Unipe uelewa, nami nitazishika sheria zako; nitazitii kwa moyo wangu wote.
35 Uniongoze katika njia ya amri zako, maana ninafurahi kuenenda katika hizo.
36 Uelekeze moyo wangu kuzielekea amari za agano lako na uniweke mbali na matendo yasiyo haki tena.
37 Uyageuze macho yangu dhidi ya kutazama mambo yasiyofaa; unihuishe katika njia zako.
38 Umtendee mtumishi wako ahadi ambayo uliifanya kwa wale wanaokuheshimu wewe.
39 Uniondolee shutumu niiogopayo, maana hukumu zako za haki ni njema.
40 Tazama, nimeyatamani maagizo yako; unihuishe katika haki yako. VAV.
41 Ee Yahwe, unipe upendo wako usiokwisha na wokovu wako kulingana na ahadi yako;
42 ndipo nitakuwa na jibu kwa ajili ya yule anayenidhihaki.
43 Usiliondoe neno la kweli mdomoni mwangu, maana nimesubiri kwa ajili ya amri zako za haki.
44 Nitazitii sheria zako siku zote, milele na milele.
45 Nitaenenda salama, maana ninayatafuta maagizo yako.
46 Nitazinena amri zako thabiti mbele ya wafalme nami sitaaibika.
47 Ninafurahia katika amri zako, nizipendazo sana.
48 Nitaziinulia mikono yangu amri zako, nizipendazo; nitazitafakari sheria zako. ZAYIN.
49 Kumbuka ahadi yako kwa mtumishi wako kwa sababu umenipa tumaini.
50 Hii ni faraja yangu katika mateso: kuwa ahadi yako imeniweka hai.
51 Wenye kiburi wamenicheka, lakini sijaiacha sheria yako.
52 Nimezitafakari amri zako za haki tangu zamani, Yahwe, nami ninajifariji mwenyewe.
53 Hasira kali imenishikilia kwa sababu ya waovu wanaoikataa sheria yako.
54 Sheria zako zimekuwa nyimbo zangu katika nyumba ninayoishi kwa muda.
55 Ninalifikiria jina lako wakati wa usiku, Yahwe, na kuzishika sheria zako.
56 Hili limekuwa zoezi langu kwa sababu nimeyatii maagizo yako. HETH.
57 Yahwe ni sehemu yangu; nimeamua kuyatii maneno yake.
Zaburi 119 in Biblia ya Kiswahili