Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 119:103-131 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 119:103-131 in Biblia ya Kiswahili

103 Ni jinsi gani maneno yako ni matamu kwenye majaribu yangu, naam, matamu kuliko asali kinywani mwangu!
104 Kupitia maagizo yako ninapata utambuzi; kwa hiyo kila njia isiyo ya kweli.
105 Neno lako ni taa ya mguu miguu yangu na mwanga wa njia yangu.
106 Nimeapa na nimethibitisha, kuwa nitazitii amri za haki yako.
107 Nimeteswa sana; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika neno lako.
108 Yahwe, tafadhali pokea dhabihu yangu ya hiari ya kinywa changu, na unifundishe amri zako za haki.
109 Uhai wangu ziku zote uko mkononi mwangu, lakini bado sisahau sheria yako.
110 Waovu wamenitegea mtego, lakini sijapotea mbali na maagizo yako.
111 Nimezifanya amri za agano lako kama urithi wangu milele, maana hizo ni furaha ya moyo wangu.
112 Moyo wangu umewekwa kuzitii sheria zako milele mpaka mwisho kabisa. SAMEKH.
113 Ninawachukia watu wa kusita-sita, lakini naipenda sheria yako.
114 Wewe ni ficho langu na ngao yangu; nalingoja neno lako.
115 Ondokeni kwangu, ninyi mtendao uovu, ili niweze kuzitii amri za Mungu wangu.
116 Uniwezeshe kwa neno lako ili niweze kuishi na nisiaibike na matumaini yangu.
117 Unisaidie, nami nitakuwa salama; siki zote nitazitafakari sheria zako.
118 Wewe huwakataa wale wote wapoteao mbali na sheria zako, maana watu hao ni wadanganyifu na si wakuaminika.
119 Wewe huwaondoa waovu wa nchi kama takataka; kwa hiyo ninazipenda amri zako thabiti.
120 Mwili wangu hutetemeka kwa hofu yako, na ninaziogopa amri za haki yako. AYIN.
121 Ninafanya kilicho sahihi na haki; usiniache kwa watesi wangu.
122 Uwe mdhamini wa ustawi wa mtumishi wako; usiwaache wenye kiburi wanionee.
123 Macho yangu yanachoka kwa kuusubiri wokovu wako na neno lako la haki.
124 Mwoneshe mtumishi wako uaminifu wa agano lako, na unifundishe sheria zako.
125 Mimi ni mtumishi wako; unipe uelewa ili niweze kuzijua amri za agano lako.
126 Ni wakati wa Yahwe kutenda, kwa maana watu wamevunja sheria yako.
127 Hakika ninazipenda amri zako kuliko dhahabu, naam, kuliko dhahabu safi.
128 Hivyo ninayafuata maagizo yako yote kwa makini, na ninachukia kila njia ya uongo. PE.
129 Sheria zako ni za ajabu, ndiyo sababu ninazitii.
130 Ufafanuzi wa maneno yako huleta nuru; na kumpa ufahamu mjinga.
131 Ninafungua kinywa changu na kutweta, maana ninazitamani amri zako.
Zaburi 119 in Biblia ya Kiswahili