Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yoshua 10:32-41 in Swahili (individual language)

Help us?

Yoshua 10:32-41 in Biblia ya Kiswahili

32 Yahweh aliitia Lakishi katika mkono wa Israeli. Yoshua aliiteka katika siku ya pili. Alishambulia kwa upanga kilia kiumbe hai kilichokuwa ndani yake, kama vile aliyokuwa amefanya huko Libna.
33 Kisha Horamu, mfalme wa Gezeri alikwea ili kuisaida Lakishi. Yoshua alimshambulia yeye na jeshi lake mpaka pale ambapo hapakuwa na mtu hata mmoja aliyesalia.
34 Baada ya hapo, Yoshua na Israeli wote walitoka Lakishi na kwenda Egloni. Walipiga kambi karibu yake na kisha wakafanya vita dhidi yake,
35 na siku hiyo hiyo wakaiteka. Waliupiga kwa upanga na waliteketeza kila mtu ndani yake kama vile Yoshua alivyofanya huko Lakishi.
36 Kisha Joshua na Israeli wote wakatoka Egloni na kwenda Hebroni. Wakainua vita dhidi yake.
37 Waliuteka mji na kuwaua kwa upanga watu wote ndani yake pamoja na mfalme wake, kujumuisha na vijiji vyote vilivyoizunguka. Waliteketeza kabisa kila kiumbe hai ndani yake, hawakuacha hata mtu mmoja aliyesalia, ni sawa sawa na vile Yoshua alivyoitenda Egloni. Aliiteketeza kabisa, na kila kiumbe hai ndani yake.
38 Baada ya hapo, Yoshua alirudi pamoja na jeshi lote la Israeli pamoja naye, wakasafiri kwenda Debiri na kufanya vita dhidi yake.
39 Aliuteka mji na mfalme wake, pamoja na vijiji vyake vya jirani. Waliwaua wote kwa upanga na waliteketeza kila kiumbe hai ndani yake. Joshua hakuacha hata mmoja hai, kama alivyokuwa amefanya kwa Hebroni na mfalme wake, na kama alivyokuwa amefanya kwa Libna na mfalme wake.
40 Yoshua aliishinda nchi yote, nchi ya milima, Negevu, nchi, nchi ya tambarare na nchi ya miteremko. Hakuna hata mfalme moja aliyebaki hai kati ya wafalme wake wote. Kwa kweli aliteketeza kila kiumbe hai, kama ambavyo Yahweh, Mungu wa Israeli alivyomwaagiza.
41 Yoshua aliwaua kwa upanga kutoka Kadeshi Barnea hadi Gaza, na nchi yote ya Gosheni hata Gibeoni.
Yoshua 10 in Biblia ya Kiswahili