Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yoshua 10:27-36 in Swahili (individual language)

Help us?

Yoshua 10:27-36 in Biblia ya Kiswahili

27 Ilipokuwa jioni, Yoshua alitoa maagizo, nao waliwashusha chini ya miti na kisha wakawatupa katika pango ambalo walikuwa wamejificha wao wenyewe. Waliweka mawe makubwa juu ya mlango wa pango. Mawe hayo yapo pale hadi leo hii.
28 Na kwa namna hii, katika siku hiyo Yoshua aliuteka mji wa Makeda na aliwaua watu wote huko kwa upanga, pamoja na mfalme wake. Aliwateketeza wote kabisa pamoja na kila kiumbe hai kilichokuwa huko. Hakuna hata mmoja aliyesalia. Alichomfanyia mfalme wa Makeda ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
29 Yoshua na Israeli wote waliipita Makeda na kufika Libna. Na huko waliingia katika vita dhidi ya Libna.
30 Yahweh pia aliitia katika mkono wa Israeli pamoja na mfalme wake. Yoshua alishambulia kila kiumbe hai ndani yake kwa upanga. Hakuacha hai hata mtu mmoja. Alichomfanyia mfalme ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
31 Baadaye Yoshua na Israeli wote pamoja naye walipanda kutoka Libna na kwenda Lakishi. Alipiga kambi karibu yake na wakafanya vita dhidi yake.
32 Yahweh aliitia Lakishi katika mkono wa Israeli. Yoshua aliiteka katika siku ya pili. Alishambulia kwa upanga kilia kiumbe hai kilichokuwa ndani yake, kama vile aliyokuwa amefanya huko Libna.
33 Kisha Horamu, mfalme wa Gezeri alikwea ili kuisaida Lakishi. Yoshua alimshambulia yeye na jeshi lake mpaka pale ambapo hapakuwa na mtu hata mmoja aliyesalia.
34 Baada ya hapo, Yoshua na Israeli wote walitoka Lakishi na kwenda Egloni. Walipiga kambi karibu yake na kisha wakafanya vita dhidi yake,
35 na siku hiyo hiyo wakaiteka. Waliupiga kwa upanga na waliteketeza kila mtu ndani yake kama vile Yoshua alivyofanya huko Lakishi.
36 Kisha Joshua na Israeli wote wakatoka Egloni na kwenda Hebroni. Wakainua vita dhidi yake.
Yoshua 10 in Biblia ya Kiswahili