Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yoshua 10:18-30 in Swahili (individual language)

Help us?

Yoshua 10:18-30 in Biblia ya Kiswahili

18 Yoshua akasema, “Viringisheni mawe makubwa katika mlango wa pango na muweke wanajeshi hapo ili kuwalinda.
19 Msibaki na kukaa nyie wenyewe. Bali wafuatilieni maadui zenu na kuwashumbulia kutokea kwa nyuma. Msiwaruhusu kuingia katika miji yao, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu amewatia katika mkono wenu.”
20 Yoshua na wana Waisraeli walikuwa wamemaliza kuwaua kwa mauaji makubwa sana, mpaka pale walipokuwa wameteketezwa kabisa; watu wachache tu walipona waliotoroka walifika miji ya ngome.
21 Kisha jeshi lote lilirudi kwa Yoshua likiwa na amani katika kambi huko Makeda. Na hakuna hata mmoja aliyethubutu kusema hata neno moja kinyume na watu wa Israeli.
22 Kisha Yoshua akasema, “Fungueni mlango wa pango, watoeni nje na waleteni kwangu hawa wafalme watano.”
23 Walifanya kama Yoshua alivyosema. Waliwaleta wafalme watano kutoka katika pango - mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi na mfalme wa Egloni.
24 Na walipowaleta wafalme kwa Yoshua, alimwita kila mtu wa Israeli, na aliwaambia maakida wa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani pamoja naye “Kanyageni miguu yenu juu ya shingo zao.” Basi walikuja na kukanyaga miguu yao juu ya shingo zao.
25 Kisha akawaambia, 'Msiogope wala kufadhaika. uwe na moyo mkuu na jasiri. Na hiki ndicho Mungu atakachokifanya kwa maadui wenu wote ambao mtapigana nao'.
26 Kisha Yoshua akawashambulia na kuwaua wafalme. Aliwatundika wote watano juu ya miti. Waliwatundika juu ya miti hata jioni.
27 Ilipokuwa jioni, Yoshua alitoa maagizo, nao waliwashusha chini ya miti na kisha wakawatupa katika pango ambalo walikuwa wamejificha wao wenyewe. Waliweka mawe makubwa juu ya mlango wa pango. Mawe hayo yapo pale hadi leo hii.
28 Na kwa namna hii, katika siku hiyo Yoshua aliuteka mji wa Makeda na aliwaua watu wote huko kwa upanga, pamoja na mfalme wake. Aliwateketeza wote kabisa pamoja na kila kiumbe hai kilichokuwa huko. Hakuna hata mmoja aliyesalia. Alichomfanyia mfalme wa Makeda ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
29 Yoshua na Israeli wote waliipita Makeda na kufika Libna. Na huko waliingia katika vita dhidi ya Libna.
30 Yahweh pia aliitia katika mkono wa Israeli pamoja na mfalme wake. Yoshua alishambulia kila kiumbe hai ndani yake kwa upanga. Hakuacha hai hata mtu mmoja. Alichomfanyia mfalme ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
Yoshua 10 in Biblia ya Kiswahili