Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yoshua 10:16-23 in Swahili (individual language)

Help us?

Yoshua 10:16-23 in Biblia ya Kiswahili

16 Basi wale wafalme watano walikuwa wametoroka na kujificha wao wenyewe katika pango huko Makeda.
17 Taarifa zilimfikia Yoshua kusema, “Wafalme watano wamepatikana wamejificha katika pango huko Makeda!”
18 Yoshua akasema, “Viringisheni mawe makubwa katika mlango wa pango na muweke wanajeshi hapo ili kuwalinda.
19 Msibaki na kukaa nyie wenyewe. Bali wafuatilieni maadui zenu na kuwashumbulia kutokea kwa nyuma. Msiwaruhusu kuingia katika miji yao, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu amewatia katika mkono wenu.”
20 Yoshua na wana Waisraeli walikuwa wamemaliza kuwaua kwa mauaji makubwa sana, mpaka pale walipokuwa wameteketezwa kabisa; watu wachache tu walipona waliotoroka walifika miji ya ngome.
21 Kisha jeshi lote lilirudi kwa Yoshua likiwa na amani katika kambi huko Makeda. Na hakuna hata mmoja aliyethubutu kusema hata neno moja kinyume na watu wa Israeli.
22 Kisha Yoshua akasema, “Fungueni mlango wa pango, watoeni nje na waleteni kwangu hawa wafalme watano.”
23 Walifanya kama Yoshua alivyosema. Waliwaleta wafalme watano kutoka katika pango - mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi na mfalme wa Egloni.
Yoshua 10 in Biblia ya Kiswahili