Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Waamuzi 16:20-28 in Swahili (individual language)

Help us?

Waamuzi 16:20-28 in Biblia ya Kiswahili

20 Alisema, “Wafilisti wako juu yako, Samsoni!” Aliamka nje ya usingizi wake akasema, “Nitatoka nje kama nyakati nyingine na kujiweka huru.” Lakini hakujua kwamba Bwana amemwacha.
21 Wafilisti walimkamata na kumng'oa macho. Wakampeleka Gaza na kumfunga kwa shaba. Alikuwa akisaga ngano katika gerezani.
22 Lakini nywele juu ya kichwa chake zilianza kukua tena baada ya kunyolewa.
23 Watawala wa Wafilisti walikusanyika ili kutoa dhabihu kubwa kwa Dagoni mungu wao, na kufurahi. Walisema, “mungu wetu amemshinda Samsoni, adui yetu, na kumtia katika ufahamu wetu.”
24 Watu walipomwona, walimsifu mungu wao, kwa sababu walisema, “mungu wetu ameshinda adui yetu na kutupa sisi - mharibifu wa nchi yetu, ambaye aliwaua wengi wetu.”
25 Walipokuwa wakisherehekea, wakasema, 'Mwite Samsoni, aje kutufurahisha.' Walimwita Samsoni nje ya jela na akawafanya wacheke. Walimsimamisha katikati ya nguzo.
26 Samsoni akamwambia yule kijana ambaye alikuwa ameshika mkono wake, 'Niruhusu nishike nguzo zilizoshikilia nyumba hii, ili nipate kuegemea.”
27 Sasa nyumba ilikuwa imejaa wanaume na wanawake. Watawala wote wa Wafilisti walikuwa huko. Juu ya paa kulikuwa na wanaume na wanawake elfu tatu, ambao walikuwa wakiangalia wakati Samsoni alipokuwa akiwafurahisha.
28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, “Bwana MUNGU, nipe nia! Tafadhali niimarishe mara moja tu, Mungu, ili nipate kulipiza kisasi kwa Wafilisti kwa kuchukua macho yangu mawili.
Waamuzi 16 in Biblia ya Kiswahili