Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 27:12-20 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 27:12-20 in Biblia ya Kiswahili

12 Mtu mwenye busara huiona taabu na kujificha mwenyewe, lakini mjinga huendelea mbele na kuteseka kwa ajili ya taabu.
13 vazi kama mwenyewe anaweka pesa kama dhamana kwa deni la mgeni; lichukue kama anaweka dhamana kwa malaya.
14 Anayempa jirani yake baraka kwa sauti ya juu mapema asubuhi, baraka hiyo itafikiriwa kuwa laana!
15 Mke mgomvi ni kama siku ya manyunyu ya mvua ya daima;
16 kumzuia ni kama kuuzuia upepo, au kujaribu kushika mafuta kwa mkono wako wa kulia.
17 Chuma hunoa chuma; kwa njia ile ile; mtu humnoa rafiki yake.
18 Yule anayeutunza mtini atakula matunda yake, na yule mwenye kumlinda bwana wake ataheshimiwa.
19 Kama maji yanavyoakisi taswira ya sura ya mtu, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwaksi mtu.
20 Kama kuzimu na Uharibifu havitosheki, ndivyo yalivyo macho ya mtu hayawezi kutosheka.
Mithali 27 in Biblia ya Kiswahili