Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 1:3-10 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 1:3-10 in Biblia ya Kiswahili

3 ili mpate maarifa kwa ajili ya kuishi kwa kutenda wema, haki na adili.
4 Mithali hizi zinatoa hekima kwa wale ambao hawakufunzwa, na kuwapa vijana maarifa na hadhari.
5 Watu wenye busara wasikie na kuongeza elimu yao na watu wenye ufahamu wapate mwongozo,
6 kwa kuelewa mithali, misemo, vitendawili na maneno ya wenye busara.
7 Hofu ya Yehova ni chanzo cha maarifa- wapumbavu hudharau hekima na nidhamu.
8 Mwanangu, sikia fundisho la baba yako na wala usiziache kanuni za mama yako;
9 zitakuwa kilemba cha neema katika kichwa chako na jebu zinazoning'inia kwenye shingo yako.
10 Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi katika dhambi zao, kataa kuwafuata.
Mithali 1 in Biblia ya Kiswahili