Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 1:13-27 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 1:13-27 in Biblia ya Kiswahili

13 Tutapata vitu vyote vya thamani; tutazijaza nyumba zetu vile tunavyoiba kwa wengine.
14 Weka vitu vyako kwetu; tutakuwa na mfuko moja kwa pamoja.”
15 Mwanangu, usitembee katika njia moja pamoja nao; usiruhusu mguu wako kugusa katika mapito yao;
16 miguu ya hukimbilia mabaya na huharakisha kumwaga damu.
17 Kwa kuwa haina maana kumtegea ndege mtego wakati ndege anaona.
18 Watu hawa huvizia kujiua wenyewe—wanatega mtego kwa ajili yao wenyewe.
19 Ndivyo zilivyo njia za kila ambaye hupata utajiri kwa udhalimu; mapato ya udhalimu huondoa uhai wa wenye utajiri.
20 Hekima inalia kwa sauti mtaani, inapaza sauti katika viwanja;
21 katika mitaa inalia kwa sauti kuu, kwenye maingilio ya milango ya mji inasema
22 “Mpaka lini enyi wajinga mtapenda kuwa wajinga? Mpaka lini enyi wenye dhihaka mtapenda dhihaka, na hadi lini enyi wapumbavu, mtachukia maarifa?
23 Zingatia karipio langu; nitatoa mawazo yangu kwa ajili yenu; nitawafahamisha maneno yangu.
24 Nimeita, nanyi mkakataa kusikiliza; nimeunyosha mkono wangu, wala hakuna aliyezingatia.
25 Lakini mumedharau mafundisho yangu yote na wala hamkuzingatia maelekezo yangu.
26 Nitacheka katika taabu yenu, nitawadhihaki wakati wa kupatwa taabu-
27 hofu ya kutisha itawapata kama tufani na maafa yatawakumba kama upepo wa kisulisuli, taabu na uchungu vitawapata.
Mithali 1 in Biblia ya Kiswahili