2 Tena, si vizuri kuwa na hamu bila maarifa na mwenye kukimbia haraka sana hukosea njia.
3 Upuuzi wa mtu unaharibu maisha yake na moyo wake hughadhabika dhidi ya Yehova.
4 Utajiri huongeza marafiki wengi, bali mtu masikini hutengwa na rafiki zake.
5 Shahidi wa uongo hatakosa adhabu na mwenye kupumua uongo hataokoka.
6 Wengi wataomba fadhila kutoka kwa mtu mkarimu na kila mtu ni rafiki wa yule anayetoa zawadi.
7 Mtu masikini huchukiwa na ndugu zake wote; je marafiki wengi kiasi gani hujitenga kutoka kwake! Anawaita, lakini wameondoka.
8 Anayepata hekima huyapenda maisha yake mwenyewe; yeye atunzaye ufahamu atapata kilicho chema.
9 Shahidi wa uongo hatakosa kuadhibiwa, bali mwenye kupumua uongo ataangamia.
10 Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa- wala kwa mtumwa kutawala juu ya wafalme.
11 Busara humfanya mtu achelewe kukasirika na utukufu wake ni kusamehe kosa.
12 Ghadhabu ya mfalme ni kama muungurumo wa simba kijana, bali fadhila yake ni kama umande kwenye majani.
13 Mwana mpumbavu ni uharibifu kwa baba yake na mke mgomvi ni maji yanayochuruzika daima.
14 Nyumba na utajiri ni urithi kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Yehova.
15 Uvivu unamtupa mtu kwenye usingizi mzito, bali asiyetamani kufanya kazi atakwenda njaa.
16 Yeye anayetii amri huyaongoza maisha yake, bali mtu asiyefikiri juu ya njia zake atakufa.