Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 19:13-28 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 19:13-28 in Biblia ya Kiswahili

13 Mwana mpumbavu ni uharibifu kwa baba yake na mke mgomvi ni maji yanayochuruzika daima.
14 Nyumba na utajiri ni urithi kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Yehova.
15 Uvivu unamtupa mtu kwenye usingizi mzito, bali asiyetamani kufanya kazi atakwenda njaa.
16 Yeye anayetii amri huyaongoza maisha yake, bali mtu asiyefikiri juu ya njia zake atakufa.
17 Mwenye ukarimu kwa masikini humkopesha Yehova na atalipwa kwa kile alichofanya.
18 Mrudi mwanao wakati kuna matumaini na usiwe na shauku ya kumweka katika mauti.
19 Mtu mwenye hasira kali lazima alipe adhabu; kama ukimwokoa, utafanya hivyo mara mbili.
20 Sikiliza ushauri na ukubali maelekezo, ili uweze kuwa na hekima mwishoni mwa maisha yako.
21 Moyoni mwa mtu kuna mipango mingi, bali kusudi la Yehova ndilo litakalo simama.
22 Shauku ya mtu ni uaminifu na mtu masikini ni bora kuliko muongo.
23 Kumheshimu Yehova huwaelekeza watu kwenye uzima; mwenye nayo atashibishwa na hatadhurika kwa madhara.
24 Mtu goigoi huuzika mkono wake ndani ya dishi; hataurudisha juu ya kinywa chake.
25 Kama utampiga mwenye mzaha, wajinga watakuwa na hekima; mwelekeze mwenye ufahamu, naye atapata maarifa.
26 Anayempora baba yake na kumfukuza mama yake ni mwana anayeleta aibu na shutuma.
27 Mwanangu, kama utaacha kusikiliza maelekezo, utapotea kutoka kwenye maneno ya maarifa.
28 Shahidi mpotofu huidhihaki haki na kinywa cha waovu humeza uovu.
Mithali 19 in Biblia ya Kiswahili