Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Mithali 10:10-31 in Swahili (individual language)

Help us?

Mithali 10:10-31 in Biblia ya Kiswahili

10 Yeye ambaye hukonyeza kwa jicho lake huleta majonzi, bali mpumbavu mwenye maneno mengi atatupwa chini.
11 Kinywa cha mwenye kutenda haki ni kama chemchemi ya maji ya uzima, bali kinywa cha uovu hufunikwa kwa jeuri.
12 Chuki huchochea mafarakano, bali upendo hufunika juu ya makwazo yote.
13 Hekima inapatikana kwenye kinywa cha mtu mwenye ufahamu, bali fimbo ni kwa ajili ya mgongo wa yule asiye na akili.
14 Watu wenye hekima hutunza maarifa, bali kinywa cha mpumbavu huleta uharibifu karibu.
15 Mali ya mtu tajiri ni mji wake mwenye ngome; ufukara wa masikini ni uharibifu wao.
16 Mshahara wa watenda haki huelekea kwenye uzima; manufaa ya waovu huelekea dhambini.
17 Kuna njia kwenda kwenye uzima kwa yule anayefuata maongozo, bali anayekataa maonyo hupotea.
18 Yeye afichaye chuki anamidomo ya uongo, na yeye anayesambaza kashfa ni mpumbavu.
19 Katika maneno mengi, hapakosi uhalifu, bali aliyemwangalifu katika usemi wake ni mwenye busara.
20 Ulimi wa yule atendaye haki ni fedha safi; kuna thamani ndogo katika moyo wa mbaya.
21 Midomo ya yule atendaye haki huwastawisha wengi, bali wapumbavu hufa kwa sababu ya kukosa akili.
22 Zawadi njema za Yehova huleta utajiri na haweki maumivu ndani yake.
23 Uovu ni mchezo achezao mpumbavu, bali hekima ni furaha kwa mtu mwenye ufahamu.
24 Hofu ya mwenye uovu humkumba ghafla, bali shauku ya mwenye haki itatimizwa.
25 Waovu ni kama dhoruba inayopita, na hawapo tena, bali mwenye haki ni msingi unaodumu milele.
26 Kama siki kwenye meno na moshi kwenye macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.
27 Hofu ya Yehova huongeza maisha, bali miaka ya waovu itakuwa mifupi.
28 Matumaini ya wale watendao haki ndiyo furaha yao, bali miaka ya waovu itakuwa mifupi.
29 Njia ya Yehova huwalinda wale wenye uadilifu, bali kwa waovu ni uhalibifu.
30 Wale watendao haki hawataondolewa, bali waovu hawatabaki katika nchi.
31 Katika kinywa cha wale watendao haki hutoka tunda la hekima, bali ulimi wa kupotosha utakatwa.
Mithali 10 in Biblia ya Kiswahili